NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma


NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi, wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma


KAIMU Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Maadili,Bw.Ally Abdul Ngowo,akizungumza wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma



NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma,kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 17 had 18,2024 jijini Dodoma


Na Okuly Julius - DODOMA


SERIKALI imeonya ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa umma ikiwemo mmomonyoko wa maadili ikiwemo viashiria vya mapenzi ya jinsia moja na mavazi yasiyofaa kwa watumishi wa umma jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya serikali.


Hayo yamesemwa leo Oktoba 17,2024 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma.


Bw.Daudi amesema kuwa Ofisi imeanza kupokea tuhuma na malalamiko kuhusu kuwepo kwa viashiria vya mmomonyoko wa Maadili kinyume na mila na desturi za nchi yetu vinavyohusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watumishi wa umma.


Amesema kuwa, vitendo hivyo ni miongoni mwa vitendo vya kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi lakini pia ni vitendo vya kinyume na maadili kwa mujibu wa miongozo ya utumishi wa umma.

"Hivyo, tumieni kikao kazi hiki, kujadili na kubadilishana uzoefu ili kuja na mapendekezo ya namna sahihi ya kudhibiti vitendo hivi na namna sahihi ya kushughulikia masuala haya yatakapojitokeza katika maeneo yenu ya kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohusishwa navyo ili kuepuka kuchafua taswira ya utumishi wa umma kwa ujumla,"amesema Bw.Daudi

Aidha ameziomba taasisi za Dini nchini kusimamia maadili na kuonya na kukemea vitendo hivyo vya ndoa ya jinsia moja katika jamii ya kitanzania mana wao wana nguvu na Sauti kubwa ya kusikika zaidi.

"Hivi sasa zipo nchi zimeacha kuzaliana kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo vya mapenzi ya jinsia moja,,Tanzania hatutaki kufika huko ndio mana tunakemea,"amesema

Kuhusu mavazi yasiofaa ameelekeza watumie waraka namba 6 wa utumishi wa umma unaozungumzia mavazi kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaochafua taswira ya serikali kwa kuvaa hovyo ndani na nje ya utumishi.

Amesema kuwa zipo taasisi ambazo viongozi wake wameanza kulegalega kwa kutochukua hatua na kuacha watumishi wakivaa mavazi kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.

"Nawaagiza kutumia waraka namba sita nasisitiza kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaovaa mavazi yasiyofaa na kuweka mkazo katika hilo , msisite kuchukua hatua mana yanachafua taswira nzima ya utumishi wa umma,"amesema

Amesema Ofisi imekuwa ikipokea mrejesho kutoka kwa wananchi tunaowahudumia, kuhusu hali isiyoridhisha ya mavazi kwa watumishi wetu wa umma.

Kwa msingi huo, tumieni kikao hiki kupitia Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 6 wa mwaka 2020 kuhusu Mavazi kwa Watumishi wa Umma, ili kujengeana uwelewa wa pamoja kupitia uzoefu mtakaobadilishana baina yenu kuhusu utekelezaji wa Waraka huo kwa watumishi waliopo kwenye maeneo yenu,.

"Na muweze kuchukua hatua ipasavyo kwa wanaokiuka Waraka husika ikizingatiwa kuwa, mwonekano wa watumishi wa umma wanapotoa huduma unabeba taswira ya taasisi, utumishi wa umma na Serikali kwa ujumla;,"amesema

Aidha amewataka Watumishi wa umma wa kada za afya na ardhi kuachana na vitendo vilivyo kinyume na maadilii ya taaluma zao ikiwemo rushwa na kuwajibu vibaya wananchi wakati wa utoaji wa huduma.

Amesema kuwa kumekuwepo na taarifa za malalamiko mengi kutoka vyanzo mbalimbali, yatokanayo na vitendo vya ukikuwaji wa maadili ya utendaji na maadili ya kitaaluma katika utumishi wa umma.

"Malalamiko hayo yamekuwa yakiwahusisha baadhi ya watumishi wetu wa umma kutoka kada mbalimbali wakiwepo Wauguzi, Madaktari, Waalimu, Maafisa Utumishi, Maafisa Ardhi, Wahasibu katika Halmashauri, Wataalam waliopo Sekta ya Ugavi wa Umeme, na Maji, pamoja na Wahandisi wanaosimamia miradi ya maendeleo. "amesema

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Maadili,Bw.Ally Abdul Ngowo,amesema wanatarajia kupokea taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Septemba 2023 hadi Septemba 2024 katika maeneo yao kuhusu suala la maadili.

"Kwa hiyo Kila Taasisi au Kila mshiriki atapata nafasi kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wake na amefanya nini katika eneo lake kuhusu suala la maadili katika kipindi hicho."amesema

 


Kamati Tendaji ya Utekelezaji wa Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa (SOFF) imekutana kwa mara kwanza katika ukumbi wa hoteli ya Morena, Morogoro, tarehe 16 Oktoba 2024, ikiwa na lengo la kupitia na kuidhinisha nyaraka muhimu za kuanza rasmi utekelezaji wa Mradi huo nchini Tanzania.

Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a aliwashukuru wajumbe wa kamati tendaji kwa kukubali kuwa sehemu ya kusimamia utekelezaji wa Mradi wa SOFF Tanzania. 

Aidha, Dkt. Chang’a alitoa shukrani zake za dhati kwa Sekretarieti ya SOFF na WMO kwa kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa wanufaika wa ufadhili wa fedha za Mfuko huo takribani dola za kimarekani milioni 9.

"Uwepo wenu ni ushahidi tosha wa dhamira yenu ya kusaidia kuboresha huduma za hali ya hewa kwa nchi yetu, kikanda na Duniani kote, huduma ambazo zitaenda kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi”, alisema Dkt. Chang'a.

Aidha, Dkt. Chang'a aliongeza kuwa uanzishwaji wa mradi wa SOFF utasidia nchi kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa data za hali ya hewa na mfumo wa mawasiliano wa ubadilishanaji wa data hizo kimataifa kwa kuwezesha masuala ya muhimu ya kiufundi na kifedha.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Ndg. Shigeki Komatsubara alieleza jinsi anavyoridhishwa na uongozi mzuri na utendaji kazi wa TMA na wataalamu wake kwa ujumla, na kuifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa katika bara la Afrika.

Aidha, alisisitiza kuwa mradi wa SOFF utatoa msaada endelevu wa uendeshaji na matengenezo na usimamizi kwa vituo vya hali ya hewa vitakavyojengwa kuwa katika hali nzuri na endelevu kwa muda mrefu kwa kuwa UNDP imejipanga kikamilifu katika kufikia malengo na mafanikio hayo.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Bi Clara Makenya aliendelea kusisitiza umuhimu mkubwa wa kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha huduma za hali ya hewa. 

Bi Clara pia alifafanua jukumu la UNEP katika kufanikisha mradi huo, ikiwa ni pamoja na kusimamia viwango vya ubora katika utekelezaji wa mradi hususan eneo la mazingira kwa kuratibu na kutoa ushauri pale inapobidi kwa maendeleo endelevu ya nchi na dunia kwa ujumla.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mha. Cyprian Luhemeja amekipongeza Chuo Kikuu  cha Kilimo Sokoine (SUA) kwa namna ambavyo kimekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha programu mbalimbali ambazo zinawasaidia wahitimu wake kujiajiri.

Ameyasema hayo wakati wa halfa ya ugawaji wa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao chuoni hapo mkoani Morogoro . Mha. Luhemeja  amesema kizazi cha leo lazima kiweke dhamira ya dhati katika elimu ili kuweza kutengeneza mustakabali wa Taifa.

Mha. Luhemeja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ugawaji wa zawadi hizo kuelekea kwenye mahafali ya 44 ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika kesho Oktoba 17,2026 ambapo wahitimu 3,060 wanatarajia kuhitimu masomo yao.

“Tutoe elimu bora na inayofaa ili kusaidia kizazi kijacho kipata ujuzi na maarifa muhimu ya kustawi katika ulimwengu unaobadilika kila mara na lazima uwe na ndoto, lakini kumbuka ndoto bila lengo ni kazi bure.

“Lazima kuchukua uchambuzi wa kina ndani yako na kuangalia nini kinakusaidia katika kufanikiwa. Mustakabali wa Taifa hili unakutegemea wewe.  Hakuna kisingizio cha kutojaribu. Usiruhusu kushindwa kwako kukufafanulie wewe ulivyo, bali acha kushindwa kwako kukufundishe,” amesema Mha. Luhemeja. 

Aliongeza kuwa SUA ni moja ya vyuo vikuu vinavyoongoza katika ukanda wetu katika kutoa elimu bora, hivyo lazima kiendelee kutathmini jinsi wahitimu wanavyojiandaa kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo.

“Serikalini tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira kwa vijana. Serikali ya Awamu ya Sita inalenga kubuni nafasi za ajira zaidi ya milioni 8 katika miaka mitano ijayo. Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine  kina jukumu muhimu la kulea wahitimu ambao sio watafuta kazi tu bali pia waundaji wa kazi. 

“Niipongeze SUA kwa mipango yake ikiwemo kuhimiza ujasiriamali na kuwapa wanafunzi ujuzi muhimu wa kujiajiri kwani juhudi hizi ni za kupongezwa na muhimu katika kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana.

Amesisitiza kwa kuwapongeza SUA namna inavyoshiriki katika mapitio ya mitaala yake ambapo amesema kwa kufanya hivyo inaonyesha kujitolea na kuhakikisha kwamba elimu yake inasalia kuwa muhimu na kuwiana na mahitaji ya soko la kazi la leo.

 


Mkurugenzi Msalala Rose Manumba ameawataka wataalam wa Halmashauri ya Msalala kuongeza weredi katika kuwatumikia wanachi ndani ya  maeneo yao ya kazi.

DED Manumba  ameyasema hayo alipofanya kikao kazi na wataalamu  kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambapo aliwasisitiza kuongeza juhudi na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao ya kazi sambamba na kusimamia miradi inayo anzishwa kwa fedha za Serikali.

Sanjari na hilo pia aliwataka wataalamu hao kuwa mfano katika maeneo yao kwa kuhakikisha wanajiandikisha katika daftari la mpigakura  Serikali za Mitaa na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kujiandikisha kwa jamii inayo wazunguka.








 


Jina langu ni Hamadi Murimi, mwanamume ambaye maisha yake ni shuhuda wa ukweli kwamba kila chaguo tunalofanya katika maisha huturudia na wakati mwingine kuamua hatima yetu bila ya sisi hata kupenda.

Kwa muongo mmoja, nilibarikiwa kuwa na mwanamke mmoja mzuri ajabu sana ambaye kusema kweli alikuwa ni mwanga wa upendo na utulivu katika maisha yangu.

Hata hivyo, kutokana na udhaifu kama mwanaume kuna wakati nilipotoka na kutoka kwenye njia. Nilimsaliti, na kwa kufanya hivyo, nilivunja utakatifu wa ndoa yetu.

Kubainika kwa uovu wangu huo ambao ulipelekea kupata watoto wawili nje ya ndoa, kuliashiria mwanzo wa anguko

Siku ambayo mke wangu alifichua siri yangu ndiyo siku ambayo uaminifu wangu kwake ulianguka rasmi. Alikuwa amehuzunika, moyo wake ukiwa umepasuliwa kwa usaliti wangu, alivunja ndoa yetu na kuondoka katika nyumba tuliyojenga pamoja.

Baada ya kuondoka kwake, nilighubikwa na majuto bila kujua ni kipi cha kufanya katika hali hiyo mbaya zaidi ambayo ilikuwa ndio mara ya kwanza kunipata katika maisha yangu tangu kuzaliwa kwangu.

Siku moja nikiwa natazama taarifa ya habari katika kituo kimoja cha runinga hapa nchini, niliona tangazo la Dr Bokko likieleza kuwa moja ya huduma wanazotoa ni pamoja na kusuluhisha migogoro ya kifamilia na ndoa.

Nilichua namba zao na kuwasiliana nao mara moja, nilimueleza shida yangu na aliweza kuniita ofisini kwake kwa ajili ya mazunguzo, nilieleza yote yaliyojiri bila kificho chochote kile, sikutaka kuwa muongo maana tayari nipo kwenye matatizo.

Walinifanyia matambiko na kunipa uchawi wa mapenzi kisha kunihakikishia ndani ya siku chache mambo yatakaa sawa. Walisema watu wengi wamepona na kupata suluhisho la changamoto zao kupitia wao, hivyo nisiwe na wasiwasi kabisa.

Baada ya siku tatu, mke wangu alirejea mwenyewe nyumbani na kusema ameamua kunisamehe kutokana na makosa yangu ambayo nilimtendea. Ilikuwa ni habari njema iliyokuja kwa ghafla sana bila kutarajia.

Sikuamini, hadi nililia machozi maana nilikuwa najua kutokana na makosa niliyomfanyia, basi ndoa yetu haiwezi kupona tena. Yaani sikuwa na matarajio yoyote kuhusu yeye. Asante sana Dr Bokko kwa msaada wako. Wasiliana naye kwa namba +255618536050.

 



Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) itahakikisha wananchi wengi mkoani Arusha wanafikiwa na huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo kupitia program yake ya tiba mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasssan.


Amesema hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayofanyika Arusha Lutheran Medical Center. (SELIAN)


Dkt. Peter Kisenge alisema kufanyika kwa kambi hiyo kunatokana na kambi ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo iliyofanyika mwezi wa sita mwaka huu jijini Arusha.


Dkt. Kisenge alisema wamerudi tena mkoani Arusha kufanya kambi ya uchunguzi na matibabu ya moyo ili kuwapima watu wenye matatizo ya moyo na kutoa elimu ya magonjwa yasiyoambukiza ambapo watu 200 sawa na asilimia 30 ya watu waliojiandikisha kwa siku mbili wamegundulika  kuwa na magonjwa ya moyo.


“Kambi ya kwanza tuliyoifanya Arusha tuliona watu 1350 tuliowakuta na matatizo ambao ni watu wazima walikuwa asilimia 14 na watoto asilimia tisa, sasa hivi asilimia imekuwa 18 ni kubwa ukilinganisha na wakati ule hii inatokana na tunaowaona hivi sasa wengi wao ni wagonjwa na wakati ule tuliona wasio wagonjwa  na wagonjwa”.


“Vitu vinavyosababisha magonjwa ya moyo ni pamoja na unywaji pombe kupitiliza, kutokula vyakula bora, kutokufanya mazoezi na uvutaji wa sigara hivyo ni vizuri wananchi wafanye mazoezi ili kupunguza kupata magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo”, alisema Dkt. Kisenge.


Alisema sababu ya pili ya kwenda Arusha ni mkoa wa utalii wanaimarisha afya ya utalii kwa watalii, watatoa elimu kwa wataalamu wa afya waliopo katika hospitali za Mt. Meru, Arusha Lutheran Medical Centre na Arusha International Conference Centre (AICC) ili waweze kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa huo.


Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu aliwaomba wananchi kujiunga na bima ya afya kwa wote pindi itakapoanza kwani gharama ya matibabu ya moyo ni kubwa lakini kama mtu akiwa na bima ya afya itampunguzia gharama ya kulipia matibabu hayo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Arusha Lutheran Medical Center Dkt. Goodwill Kivuyo aliwashukuru wataalamu wa JKCI kwa kufanya kambi ya matibabu ya moyo katika hospitali hiyo ambayo imewasaidia wananchi kupata huduma pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya wa hospitali hiyo.


Dkt. Kivuyo ambaye ni bingwa wa upasuaji aliishukuru serikali kwa kuweka mwongozo na makubaliano ya taasisi za umma hasa za hospitali ya kuanzisha mahusiano na hospitali binafsi jambo lililosababisha wananchi wengi zaidi kupata huduma za matibabu ya kibingwa.

 

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulikia Makazi (UN-HABITAT) Bi.Anaclaudia Rossbach (kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda mjini Zanzibar hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Makazi Duniani ( UN HABITAT) Anaclaudia Rossbach.

Viongozi hao walikutana hivi karibuni mjini Zanzibar katika kikao kilichohudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Bw. Deogratius Kalimenze, Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya urasimishaji makazi Bw. Nicolaus Mwakasege pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Mbaraka Abdulrahman.

Katika mazungumzo yao. Mhe. Pinda alimueleza Mkurugenzi huyo wa UN-HABITAT kuwa, Tanzania inaunga mkono juhudi zinazofanywa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika kusaidia miradi mbalimbali nchini aliyoieleza kuwa imefikia takriban dola milioni 29.3.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa, ni uwepo wa miji salama na kuzuia uhalifu, maji na usafi wa mazingira, mfuko wa kuwezesha wanawake kumiliki ardhi pamoja na mradi wa usambazaji maji ziwa victoria ambapo ameielezea miradi hiyo yote kuwa imesaidia kuboresha maisha ya watanzania.

Aidha, amemueleza mkurugenzi huyo wa UN -HABITAT nia ya Serikali kulipatia shirika hilo ofisi hapa Tanzania ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ambapo Mkurugenzi huyo amekubali ombi la shirika lake kuwa na ofisi nchini Tanzania.

" tutaendelea kutoa ushirikiano wa karibu katika miradi tofauti itakayoboresha makazi katika miji mbalimbali pamoja na mchakato mzima wa uanzishwaji ofisi ya UN-HABITAT Tanzania" alisema Anaclaudia.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulikia Makazi (UN-HABITAT) Bi. Anaclaudia Rossbach mara baada ya kikao kilichofanyika mjini Zanzibar hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulikia Makazi (UN-HABITAT) Bi. Anaclaudia Rossbach ( wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wengine mara baada ya kikao kilichofanyika mjini Zanzibar hivi karibuni.



Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeanzisha kitengo maalum kwa wagonjwa wa kiharusi ili kuhakikisha wagonjwa wa kiharusi wanapata huduma stahiki kwa haraka ikiwa ni mkakati wa kuendelea kupunguza vifo na madhara ya muda mrefu yatokanayo na ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji MNH Prof. Mohamed Janabi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuboreshwa na kuimarika kwa kliniki za magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu ikiwa ni miaka miwili tangu kliniki hizo zilipohamishiwa Muhimbili Mloganzila Oktoba, 2022.

Prof. Janabi amebainisha kuwa kitengo maalum cha kiharusi kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 10 kwa wakati mmoja na kina mashine maalum za ufuatiliaji wa mienendo ya mgonjwa kadiri anavyopatiwa matibabu ili kumuwezesha mtaalam kuchukua hatua stahiki kutokana na changamoto aliyonayo mgonjwa.

Aidha ameongeza kuwa kitengo cha ubongo na mishipa ya fahamu kimeshuhudia ongezeko la wagonjwa wa nje kutoka wastani wa wagonjwa 50 mwaka 2022 na kufikia wagonjwa 150 kwa siku ambapo katika kila wagonjwa 10, wagonjwa 6 wana kiharusi.

“Katika kukabiliana na magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu tunawahudumia wagonjwa kwa kutumia wataalam bobezi wa magonjwa wa fani mbalimbali ikiwemo wa magonjwa ya dharura, radiolojia, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, ICU na fiziotherapia” amebainisha Prof. Janabi.

Prof. Janabi amesema kuwa kitengo hicho kinatoa dawa maalum kwa magonjwa ya kutetemeka na kushindwa kutumia viungo vya mwili (Movement Disorder) kama vile mikono, miguu na shingo (Dystonia) na kutoa huduma za matibabu ya kifafa kwa watu wazima ambapo kwa kipindi cha miaka miwili wamehudumia wagonjwa 338 wa nje na wa ndani 4,850.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fhamu Dkt. Mohamed Mnacho ameishauri Jamii kuepuka unywaji wa pombe uliopitiliza kwa kwa kuwa kunaweza kuathiri seli za ubongo wa binadamu ambapo kunaweza kusababisha kiharusi.












 


Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo ameanza ziara ya kata kwa kata katika makazi ya wananchi na vijiwe vya bodaboda, bajaji na masoko kuwaelimisha umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa utaofanyika novemba 27 nchini.  

Mpogolo ameanza ziara yake ya kuhamasisha katika makutano ya barabara mataa ya kamata kata ya gerezani kuelimisha  shirikisho la vyama vya  bodaboda na bajaji pamoja na wasafiri wengine wa vyombo vya moto.  

Akizungumza na wananchi, makundi mbalimbali ya kijamii Mpogolo amewataka wananchi na makundi yote kujitokeza kujiandikisha kwa siku nne zilizosalia na kujitokeza kupiga kura.

Amesema ni muhimu kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wananchi wote wenye sifa kuanzia miaka 18 na kuendelea, mkazi halali wa  mtaa huo, mwenye akili timamu ana haki ya kujiandikisha na kupiga kura katika zoezi lililoanza tarehe 11 hadi 20 na uchaguzi ni tarehe 27 mwezi ujao.

Ameeleza kuwa umuhimu wa zoezi ili ni mkubwa kwa wananchi wote wenye sifa kujua uchaguzi wa mitaa unawahusu kuchagua viongozi wao wa mitaa wanaokua nao katika makazi yao na kusaidia kutatua kero zao za kijamii.

Amebainisha asili ya uchaguzi wa mitaa ni  kutokana na serikali kuu   kugatua madaraka kushusha katika ngazi za mitaa, vijiji na vitongoji ili wananchi wafanye maamuzi yao. 

Akiongea na wananchi wa kata ya vingunguti ,  banana ,kitunda, kitunda shule , kivule sokoni , fremu kumi, msongola, chanika, zingiziwa na gongo la mboto Mpogolo amesema wilaya ya ilala ina vituo 454 katika mitaa 159 ambavyo vinafunguliwa na kufungwa kwa wakati. 

Mpogolo amesema ushiriki wa wananchi katika uchaguzi utawasaidia kupata viongozi bora, wanaosoma mapato na matumizi, wanaofanya mikutano na kusimamia ulinzi na usalama katika mitaa yao.

Kuhusu baadhi ya watu wanaowazua wananchi wenye sifa za kujiandika kwenda vituoni Mpogolo ameliagiza jeshi la polisi Mkoa wa ilala kufanya msako wa kuwakamata na kuwafikisha mahakakamani ndani ya siku mbili.

Aidha Mpogolo ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi, halmashauri ya jiji ina zaidi ya bilioni 11 kuwakopesha makundi ya bodaboda na bajaji au mmoja mmoja kupata mikopo ya almashauri ambayo inatolewa kwa kundi la wanawake, vijana na walemavu.

Mikopo ambayo kwa sasa imeongezwa sifa kutoka umri wa miaka 35 hadi  45 tofauti na mikopo ya awali ilivyokua. 

Akizungumzia suala la barabara ya Kitunda, kivule hadi msongola amewahakikishia wananchi, wafanyabiashara, bodaboda na bajaji barabara hiyo imeshapata mkandarasi na mkataba wa ujenzi huo utashuhudiwa na Waziri wa  nchi ofisi ya Rais tawala za serikali za mikoa na mitaa Tamisemi Mohamedy Mchengerwa wakati wowote kuanzia sasa. 

Barabara ambayo itajengwa katika kiwango cha lami, mifereji, taa za barabarani na kuwa katika viwango vya kisasa ili kumaliza changamoto ya muda mrefu kwa wakazi wa kata ya kitunda, kivule na  msongola.

Mpogolo amesema maendeleo ya wananchi katika sekta ya elimu, afya, miundombinu, na maji  yanaanzia serikali za mitaa.

Kwa upande wa jeshi la polisi kupitia kwa mrakibu wake SP Kasira kwa niaba ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam amewahakikishia wananchi jeshi la polisi liko makini kuhakikisha ulinzi na usalama wakati wa kipindi cha kujiandikisha na kupiga kura unakuwa wa kutosha. 

Nae  Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya bodaboda na bajaji  Hussein Chanje ameishukuru Serikali ya awamu ya sita  ya Rais Samia kwa kuwasaidia maafisa usafirishaji kutambulika rasmi, kuingia mjini na kuongeza umri wa kuchukua mikopo kutoka miaka 35 hadi 45 hali inayofanya wafanye kazi zao kwa amani.

Umoja huo kupitia Mwenyekiti wao wamehakikisha kushiriki vilivyo kujiandikisha na kupiga kura pamoja na kuhamasisha makundi mengine. 

Huu ni mwendelezo wa Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo kuhamasisha zoezi la kujiandikisha na kupiga kura ambalo alilianzia mapema katika kata zote 36 za ilala, vijiwe vya kahawa, magazeti,  michezo na kuendelea katika masoko, vijiwe vya bajaji, bodaboda, babalishe na mamalishe.






 KAIMU Katibu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Uvccm, Bulugu Magege, amekitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuacha kulinajisi zoezi la uandikishaji wa wapiga kura linaloendelea nchini.


Akizungumza leo, Septemba 16, Jijini Dodoma, alipojiandikisha katika shule ya Dodoma Mlimani, Burugu amewasihi vijana kujitokeza kwa wingi katika mchakato huu muhimu wa kujiandikisha na kupiga kura.

Amesema kitendo cha viongozi wa Chadema kuzuia vijana wenye umri wa miaka 18 kujiandikisha kinawanyima haki zao za msingi na kikatiba.

Amesisitiza kwamba zoezi hili linasimamiwa kwa umahiri na Tamisemi, akionyesha kuridhishwa na idadi kubwa ya vituo vya kujiandikisha vilivyowekwa.

Burugu ameongeza kuwa ni muhimu kwa vijana kutumia fursa hii ili kuweza kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia na kuhakikisha sauti zao zinaskika.


Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati wameandaa Jukwaa la majadiliano  kuhusu nishati safi ya kupikia kwenye bara la Afrika ambapo limefanyika jijini Dar es Salaam katika hotel ya Hayyat.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko  kwenye uzinduzi wa mkutano wa 9 wa soko la Nishati Afrika amesema ifikapo mwaka 2030 wanatarajia takribani watu million 300 wawe wamefikiwa na nishati ya umeme bara la Afrika.

Amesema kuwa, lengo la mkutano huo ni kwenda kujadili na kufanya tafakuri kubwa kama bara juu ya upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia ambapo mfumo wake unachangamoto nyingi kwenye utekelezaji wake ikiwemo gharama ya upatikanaji.

"Watu wengi wanalalamika gharama ni kubwa ya kupata huduma hiyo, sasa ni lazima kueka mikakati mizuri ili kuhakikisha gharama za upatikanaji wake uwe rahisi na watu waweze kumudu, ambapo mitungi ya gesi laki 4 itauzwa kwa nusu bei"amesema

Aidha, amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utakua ni maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Afrika wanaokwenda kujadili masuala ya nishati kwenye bara la Afrika kwani watu 300 sio kazi  rahisi kuwapata. 

Amesema kuwa, Benki ya maendeleo ya Afrika imepima kwa vipimo vyake kwa kukaa na wadau wote ambao wanapata pesa kutoka kwao imeonekana Tanzania imepiga hatua kuwa san na wamefanikiwa jambo lililopelekea nchi hiyo kuwa shamba darasa kwa wenzao kwenye usimamizi wa Sekta ya nishati.

Aidha, amesema nchi Tanzania imepata heshima ambayo haikua kazi rahisi bali Kwa mausiano mazuri ya kidiplimasia kati ya nchi hiyo na Benki ya maendeleo ya Afrika ambapo wamekiri Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya kisera na usimamizi, uzalishaji na usafirishaji na upelekaji wa umeme Vijijini.

Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Nishati, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa kijani AFDB Dr Kevin kairuki wameamua kufanya kazi Kwa pamoja na Tanzania kwa sababu ipo mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Tanzania imekua ikitilia manani mambo ya nishati safi ndio sababu tukakaa na wadau kama vile World Benki tukasema hili kongamano lifanyike Tanzania kwani kupata watu million 300 wa kutumia nishati safi ya kupikia sio rahisi" amesema Dr Kairuki.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Eng Felchesmi Mrama amesema mkutano huo wataweza kujadiliana ukuaji wa Nishati, matarajio, namna ya kuipata uzalishaji na ujumuishaji wa Sekta binafsi kwani ifikapo 2034 nishati ipatikane kwa unafuu.