Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akitoa elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.
Na Mwandishi Wetu,TABORA
Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, leo, tarehe 6/10/2026, imekutana na wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa mkoa wa Tabora, na kuwaelimisha kuhusu haki na wajibu wao katika huduma za nishati na maji.
Wanachama hao pia wamepata elimu kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko na namna yanavyoshughulikiwa, kanuni za ubora wa huduma ya maji, matumizi sahihi na salama ya gesi ya kupikia na umuhimu mikataba ya huduma kwa wateja huku wakisisitizwa kutumia mafundi umeme wenye leseni zilizotolewa na EWURA.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Karim Ally, akifungua warsha hiyo iliyofanyika katika Ofisi za EWURA Kanda ya Magharibi, mjini Tabora, ameeleza kuwa ni utaratibu wa Mamlaka kukutana na wadau mbalimbali ikiwemo watu wenye ulemavu ili kuwaelimisha kuhusu udhibiti sanjari na kupokea mrejesho kuhusu huduma zinazodhibitiwa.
Aidha, washiriki wameiomba EWURA kuendeleza elimu hiyo kwa kuwafikia wanachama wa SHIVYAWATA katika maeneo mbalimbali nchini na pia kwa makundi mengine ya aina hiyo ili kuimarisha uelewa wao katika masuala ya kiudhibiti.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akitoa elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu-kazi, ajira na mahusiano, mhe. Deus sangu (kulia) akiteta jambo na waziri wa kazi nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mari, mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue’ kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, uliofanyika Oktoba 6, 2026, jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Husserin Ali Mwinyi (Wapili kushorto), akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Kazi wa nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mariri, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, akishuhudia wakati w aufunguzi wa mkutano wa pili wa majadiliano ya Doha (Doha Dialogue)

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza Kulia) akiwa na viongozi wenzake, katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialoguie’ Jijini Dar Es Salaaam, Oktoba 6, 2026
✅ Abainisha Makubaliano ya Mkutano huo katika kuimarisha Uhamaji wa Nguvu Kazi
Na: OWM (KAM), Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue II 2026 umefungua fursa zaidi za ajira kwa Watanzania na wananchi wa nchi nyingine za Afrika, kupitia kuimarishwa ushirikiano wa uhamaji wa nguvu kazi kati ya Afrika na nchi za Ghuba (GCC+).
Mhe. Sangu amesema hayo akizungumza na Waandishi wa Habari mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika leo Oktoba 6, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Amesema, kama taifa tumepata fursa ya nchi za GCC+ kuja nchini ili kujadili na kutafakari uhamaji wa nguvu kazi kutoka Barani Afrika kwenda katika nchi za Ghuba (GCC+).
“ Kupitia mkutano huu tumejadili na nchi mbalimbali za Ghuba kuona namna gani wanaweza kuongeza fursa za ajira ikiwemo za kitaalamu (Skilled labour) zinazohusisha madaktari, manesi, wafamasia, mafundi na mainjinia,”
Aidha, Mhe. Sangu amesema vijana wa Kitanzania waliopelekwa kwenye nchi hizo kufanya kazi wameonyesha uhodari katika kuchapa kazi na uaminifu.
Kadhalika, amesema katika mkutano huo nchi za Ghuba zimeihakikishia mkutano huo uliowaleta pamoja wajumbe kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika uzingatiaji wa mikataba waliyoingia (Bilateral Agreements) ambayo inazingatia haki na maslahi ya wafanyakazi hasa katika suala la hifadhi ya jamii.
“ Tumekubaliana kimsingi sasa, suala la hifandhi ya jamii ni kipaumbele katika mikataba yote tutakayoingia na nchi hizo, tumejadili kuhusu bima ya afya kwa wanaokwenda kufanya kazi na malipo ya mishahara,” amesema
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mawakala wa Uhamaji wa Nguvu Kazi na Ajira Bw. Abdallah Khalid Mohammed, amefurahia makubaliano hayo na kwamba kutakuwa na mfumo ambao utawezesha mfanyakazi kuhakikisha usalama wake unazingatiwa huku kila upande unawajibika.
MWISHO

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu-kazi, ajira na mahusiano, mhe. Deus sangu (kulia) akiteta jambo na waziri wa kazi nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mari, mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue’ kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, uliofanyika Oktoba 6, 2026, jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Husserin Ali Mwinyi (Wapili kushorto), akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Kazi wa nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mariri, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, akishuhudia wakati w aufunguzi wa mkutano wa pili wa majadiliano ya Doha (Doha Dialogue)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akisisitiza jambo mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, Uliofanyika Oktoba 6, 2026, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza Kulia) akiwa na viongozi wenzake, katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialoguie’ Jijini Dar Es Salaaam, Oktoba 6, 2026
Dar es Salaam, Oktoba 6, 2026
Mkutano wa Pili wa mazungumzo ya Doha (Doha Dialogue) kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, umekamilika leo Oktoba 6, 2026 jijini dar es salaam na kuja na fursa mpya za ajira kwenye nchi za Ghuba.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mwishoni mwa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema kama taifa tumepata fursa ya nchi za GCC+ kuja nchini ili kujadili na kutafakari uhamaji wa nguvu kazi kutoka Barani Afrika kwenda katika nchi za Ghuba (GCC+)
“ Lakini pia tumeahidiwa ajira zaidi, kando na mkutano huu tuliendelea na mikutano mingine kuhusisha nchi mbalimbali za Ghuba kuona namna gani wanaweza kuongeza fursa za ajira hivyo katika mikutano hiyo tumepata fursa nyingi zitakazopelekea kusaini mikataba mingi ya ajira.” amesema Mhe. Sangu.
Mbali na ajira zisizo za ujuzi (Un skilled), sasa zimekuja fursa za ajira za kitaalamu (Skilled labour) wanahitaji vijana wengi madaktari, manesi, wafamasia, mafundi na mainjinia, kwahivyo wameona fursa ya nguvu kazi kutoka afrika lakini kipekee kutoka Tanzania.
“Vijana wa Kitanzania waliopelekwa kwenye nchi hizo kufanya kazi wameonyesha uhodari katika kuchapa kazi na uaminifu,” amesisitiza.
Aidha, Mhe. Sangu amesema, katika mkutano huo nchi za Ghuba zimeuhakikishia mkutano huo uliowaleta pamoja wajumbe kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika na AU uzingatiaji wa mikataba waliyoingia (Bilateral Agreements) ambayo mingi inazingatia haki na maslahi ya wafanyakazi hasa katika suala la hifadhi ya jamii.
“ Tumekubaliana kimsingi sasa, suala la hifandhi ya jamii ni kipaumbele katika mikataba yote tutakayoingia na nchi hizo, tumejadili kuhusu bima ya afya kwa wanaokwenda kufanya kazi na malipo ya mishahara,”Amesema Mhe. Sangu.
MWISHO
📌Asisitiza mifumo iliyozinduliwa ifanye kazi kwa ufanisi na kuendana na mahitaji ya wateja
📌Aipongeza TANESCO kwa ubunifu na kuimarisha huduma kwa wateja wakubwa
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, leo Oktoba 6, 2026 amezindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliohuishwa pamoja na huduma mbalimbali za TANESCO zinazolenga kuboresha zaidi namna ya utoaji wa huduma kwa wateja kwa ufanisi na kwa wakati, uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Super Dome, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Homera amesema matumizi ya mifumo ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma kwa wateja yanazidi kuiwezesha TANESCO kupiga hatua kubwa katika kuboresha huduma zake kwa kuzingatia uwajibikaji, uwazi na weledi unaolenga kuleta matokeo chanya kiutendaji.
Ametoa rai kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi katika matumizi ya umeme zinashughulikiwa kwa haraka kwa kuwa changamoto katika huduma ya umeme zinaweza kuathiri moja kwa moja uzalishaji na shughuli za kiuchumi.
“Mwelekeo wa Serikali ni kujenga sekta ya nishati inayoweza kuunga mkono kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Tunataka kuona shughuli za uzalishaji zinaendelea bila vikwazo visivyo vya lazima na tunataka wananchi wapate huduma kwa urahisi zaidi,” ameeleza Waziri Homera.
Amesema Tanzania hivi sasa ina umeme wa kutosha, ambapo uwezo wa uzalishaji umefikia jumla ya Megawati 4,606 dhidi ya mahitaji ya juu ya Megawati 2,316, hatua inayotoa fursa zaidi za kukuza shughuli za kiuchumi kupitia uwekezaji katika viwanda, biashara na shughuli za kijamii.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mhe. Subira Mgalu, ameipongeza Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuendelea kuja na ubunifu unaolenga kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika nyanja mbalimbali.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Mhe. Balozi Zuhura Bundala, amesema Bodi itaendelea kuisimamia TANESCO katika kuhakikisha utoaji wa huduma unaenda sambamba na matumizi ya teknolojia za kisasa, ili huduma zimfikie mteja moja kwa moja bila vikwazo.
“Bodi itaendelea kuishauri TANESCO katika utoaji wa huduma kwa ufanisi. Kwetu sisi, mteja ni mfalme, na huduma inayotolewa na Shirika inamgusa mwananchi moja kwa moja. Tumejipanga kuhakikisha jitihada hizi zinaendelea kupiga hatua,” amesisitiza Balozi Bundala
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, ametoa ufafanuzi kuhusu uzinduzi wa Twiga Assistant, mfumo unaolenga kuachana na utoaji wa huduma kwa njia za makaratasi na kuingia katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki inayompunguzia mteja kutumia muda mrefu kusubiri huduma anayohitaji.
“TANESCO inafanya kazi kubwa kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi baada ya kukamilika kwa miradi mingi ya kimkakati, ukiwemo Mradi wa Chalinze–Dodoma. Hatua hii inatupa nguvu ya kuja na ubunifu wa kuona namna ya kumfikia mteja kwa haraka.
Ndiyo maana TANESCO imeamua kushuka chini na kusogeza huduma zake karibu na wananchi,” amefafanua Bw. Twange.
Hafla hiyo iliyobeba kaulimbiu ya “EXTRA MILE” imeenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya 185 kwa ajili ya wateja wakubwa, Twiga AI Chatbot, mfumo saidizi wa kidijitali unaolenga kujibu maswali ya wateja, Kitengo cha watwja wakubwa kilichoboreshwa, pamoja na Premium Customer Portal, mfumo maalumu kwa ajili ya wateja wakubwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika shughuli za Shirika.
Uzinduzi huo umefanyika katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, ikiwa ni sehemu ya jitihada za TANESCO kuendelea kuboresha huduma kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuhakikisha mteja anapata huduma kwa urahisi, haraka na kwa ufanisi.
Na Mwandishi Wetu- Same
Katibu Tawala Wilaya ya Same Bi. Mamndolwa Gembe amewataka Kamati ya Usimamizi wa Maafa Wilaya ya Same kuendelea kutoa elimu ya tahadhari kwa wananchi wa maeneo yote ya wilaya hiyo hususani wakulima na wafugaji.
Bi. Gembe amesisitiza hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, leo Octoba 06, 2026, wakati akifungua kikao kazi cha Kamati za usimamizi wa maafa za wilaya na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) sambamba na kuimarisha utoaji wa matumizi ya taarifa za tahadhari za awali katika kujiandaa na kukabiliana na madhara ya El nino.
“Wilaya ya Same ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na mabadiliko makubwa ya tabianchi, kijiografia wilaya yetu ina maeneo ya milima na tambarare, hivyo inatufanya tuwe katika hatari ya kukabiliwa na changamoto za pande mbili, kutokana na hilo mipango na mapendekezo yatakayotolewa katika kikao kazi hiki yasibaki kwenye nyaraka tu, bali yakatimizwe na kuingizwa kwenye mipango kazi ya halmashauri, mamlaka za kata na vijiji” amesisitiza Bi. Gembe.
Aidha, Bi. Gembe ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa ushirikiano lakini pia amesema kuwa Serikali ya Wilaya ya Same ipo tayari kufanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha malengo ya programu hiyo yanatimia.
“Tunawashukuru sana kwa kuchagua Wilaya ya Same kuwa sehemu yay a ziara na kikao kazi hiki cha kimkakati, ujio wenu ni Ushahidi tosh awa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kulinda Maisha na mali za wananchi dhidi ya athari za majanga Ameongeza Katibu Tawala huyo.
Nae, Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bi. Sandra Hakim amebainisha kuwa, lengo la programu hiyo ni kuifanya taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa inashuka chini ili jamii ikiwemo wazee, wamama, walemavu na watoto waweze kupata taarifa kwa wakati kwani upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa mapema zitakuwa na thamani pale utakapochukua hatua kabla ya majanga kutokea.
Katika kikao hicho mada mbalimbali kuhusu Utabiri wa Msimu, El nino na madhara tarajiwa, Dhana ya Maafa ikiwemo mzingo wa maafa, Mpango wa Dharurawa Kukabiliana na Maafa na majukumu ya kamati na utekelezaji wa mpango pamoja na Usambazaji wa Huduma za Hali ya Hewa ziliwasilishwa kwa Kamati ya Usimamizi wa Maafa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu katika ukusanyaji wa kodi hivyo yanapaswa kutiliwa mkazo ili kuongeza uwazi, kuimarisha usimamizi wa kodi na kurahisisha ulipaji kodi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo jijini Arusha Oktoba 06, 2026 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) na kueleza kuwa teknolojia ni nyenzo muhimu katika kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuimarisha huduma kwa walipa kodi ndiyo maana mkutano huo umekuja na kauli mbiu inayogusa teknolojia.
Amesema pamoja na umuhimu wa teknolojia, mafanikio katika ukusanyaji wa mapato hayawezi kutegemea teknolojia pekee, bali yanahitaji sera nzuri, madhubuti, zinazoeleweka na zinazotabirika, pamoja na usimamizi wa kodi wenye ufanisi na unaokidhi mahitaji ya walipakodi.
Makamu wa Rais pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya kodi, akibainisha kuwa biashara zinazovuka mipaka, makampuni ya kimataifa, miamala ya kidijitali pamoja na mali za kifedha zinazohifadhiwa nje ya nchi zimefanya ushirikiano kati ya mamlaka za kodi kuwa muhimu zaidi.
Amesema Tanzania inaendelea kuimarisha ushiriki wake katika ushirikiano wa kimataifa wa kodi, ikiwemo kubadilishana taarifa za kodi na kutoa msaada wa kiutawala baina ya nchi huku akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuongeza uhakika wa kodi, kubadilishana taarifa, kuzuia na kutatua migogoro ya kikodi.
Amesema uratibu mzuri kati ya nchi unaweza kusaidia kulinda mapato ya Serikali huku ukipunguza uwezekano wa kutozwa kodi mara mbili na kuondoa sintofahamu kwa wawekezaji halali.
“Nchi inayovutia uwekezaji siyo ile isiyokuwa na kodi, bali ni ile yenye kanuni za kodi zilizo wazi, thabiti na zinazosimamiwa kwa haki, zikiungwa mkono na taratibu bora za forodha na ukusanyaji wa mapato,” amesema.
Awali akizungumza katika mkutano huo Rais wa CATA Mhe. Abu Tariq Jamaluddin amesema matumizi ya teknolojia ya kisasa yamekuwa yakisaidia nchi wanachama wa CATA kurahisisha utawala wa kodi kwa kuweka mazingira rahisi ya ukusanyaji wa mapato na kuwasaidia walipakodi kufuata sheria za kodi.
Amesema kauli mbiu ya mkutano huo inalenga kuhimiza matumizi zaidi ya teknolojia na kueleza kuwa CATA itaendelea kuwezesha matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa kodi ili kuimarisha usimamizi wa kodi baina ya nchi wanachama.
Amesema kupitia mkutano huo nchi washiriki wataweza kubadilishana ujuzi na uzoefu kuhusu usimamizi wa kodi na matumizi ya teknolojia.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao ndiyo waandaaji wa mkutano huo Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo imepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ambayo yameboresha zaidi huduma za usimamizi wa kodi kwa kuongeza uwazi na ufanisi.
Amesema kupitia matumizi ya teknolojia TRA imekuja na mfumo wa IDRAS unaosimamia kodi za ndani ambao unamuwezesha Mlipakodi kutoa risiti za kielektroniki kwa kutumia simu ya mkononi bila kuwa na mashine hali ambayo imeongeza uhiari katika kulipa kodi na kupunguza kuonana kwa walipakodi na maofisa wa TRA.
Amesema kupitia mkutano huo wataweza kubadilishana ujuzi na mataifa mengine akieleza kuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa pia kwa Tanzania yameongeza wigo wa kodi kutokana na kuwapa uhuru walipakodi kujisajili kupitia mtandao na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN).
Mkutano huo utadumu mpaka Oktoba 09 mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu - ARUSHA.
Warsha hiyo ya siku tano, inayofanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026, imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) na Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA), ikiwa na lengo la kujadili namna Vituo vya Usaidizi wa Usalama wa Nyuklia (Nuclear Security Support Centres – NSSCs) vinavyoweza kusaidia nchi kujenga na kudumisha wataalamu wenye uwezo wa kusimamia masuala ya usalama wa nyuklia.
Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), ambaye pia ni Mratibu wa Kitaifa wa Tanzania na Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA) (National Liaison Officer – NLO), Prof. Najat Kassim Mohamed, amesema matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani yanahitaji kwenda sambamba na uwepo wa wataalamu wenye ujuzi na uwezo wa kuhakikisha nyenzo za nyuklia na vyanzo vingine vya mionzi vinatumika kwa uwajibikaji na kulindwa ipasavyo.
Amesema mifumo bora na vifaa vya kisasa pekee haviwezi kuhakikisha usalama wa nyuklia bila kuwa na wataalamu wenye ujuzi wa kuvitumia, kuvitunza na kuchukua hatua stahiki pale linapotokea tukio linalohusisha usalama wa nyuklia.
“Maendeleo ya rasilimali watu ni jukumu endelevu la kila nchi. Tunahitaji kutambua ujuzi unaohitajika, kujua uwezo tulionao, kutoa elimu na mafunzo yanayofaa na kutathmini kama mafunzo hayo yameleta matokeo yanayotarajiwa,” amesema Prof. Najat.
Warsha hiyo imekusanya watu 48 kutoka nchi 18, wakiwemo washiriki 25 wanaohudhuria moja kwa moja jijini Arusha, washiriki 18 wanaoshiriki kwa njia ya mtandao pamoja na wataalamu watano. Wataalamu wanaowezesha warsha hiyo wanatoka Algeria, Misri, Malaysia na Tanzania.
Prof. Najat amesema ushirikiano huo unaonesha dhamira ya pamoja ya nchi zinazoshiriki katika kujenga uwezo endelevu wa kukabiliana na changamoto za usalama wa nyuklia, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na mifumo ya kuhifadhi maarifa na kuendeleza utaalamu hata pale watumishi wanapobadilisha majukumu au kuondoka katika utumishi.
Kwa mujibu wa Prof. Najat, Vituo vya Usaidizi wa Usalama wa Nyuklia vina nafasi muhimu katika maeneo matatu yanayokamilishana, ambayo ni maendeleo ya rasilimali watu, msaada wa kiufundi na msaada wa kisayansi. Maeneo hayo yanasaidia nchi kuwa na wataalamu wenye uwezo, vifaa na mifumo inayofanya kazi kwa ufanisi pamoja na utaalamu wa kisayansi unaohitajika katika kushughulikia masuala ya usalama wa nyuklia.
Katika kipindi cha warsha hiyo, washiriki watajadili misingi ya mifumo ya usalama wa nyuklia na namna ya kuifanya iwe endelevu, nafasi ya Vituo vya Usaidizi wa Usalama wa Nyuklia katika maendeleo ya rasilimali watu, pamoja na umuhimu wa kuwa na mipango ya kitaifa ya kujenga uwezo wa wataalamu wanaohusika na usalama wa nyuklia.
Majadiliano pia yataangalia kwa kina maeneo matatu muhimu ya usalama wa nyuklia ambayo ni kuzuia matukio ya kiusalama, kugundua vitendo au matukio yanayoweza kuhatarisha usalama na kuwa na uwezo wa kuchukua hatua stahiki yanapotokea.
Mada nyingine zitakazojadiliwa ni pamoja na usimamizi na utunzaji wa maarifa ndani ya taasisi, kubaini mapungufu katika uwezo uliopo, kujenga uwezo wa kitaifa na namna ya kutekeleza mipango ya maendeleo ya rasilimali watu kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kila nchi.
Prof. Najat amewataka washiriki kutumia warsha hiyo kubadilishana uzoefu kwa uwazi, ikiwemo kueleza mafanikio, changamoto, upungufu wa rasilimali na vikwazo wanavyokutana navyo katika nchi zao ili majadiliano hayo yasaidie kupata njia zinazoweza kutekelezeka katika mazingira halisi.
Amesisitiza kuwa mafanikio ya warsha hiyo hayatapimwa kwa idadi ya mada zitakazowasilishwa pekee, bali kwa namna maarifa na uzoefu watakaoupata washiriki vitakavyosaidia kuleta maboresho katika taasisi na nchi zao baada ya kumalizika kwa warsha.
Warsha hiyo pia inatoa fursa kwa nchi zinazoshiriki kujifunza kutokana na uzoefu wa kila mmoja, kubaini mbinu zinazoweza kutumika katika mazingira tofauti na kuimarisha mahusiano ya kitaalamu yatakayosaidia kuendeleza ushirikiano katika masuala ya usalama wa nyuklia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TAEC, Bwana Peter Ngamilo, amesema kufanyika kwa warsha hiyo nchini Tanzania ni fursa muhimu ya kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa usalama wa nyuklia na kuonesha mchango wa ushirikiano wa kimataifa katika kujenga uwezo wa wataalamu wanaosimamia eneo hilo.
“Usalama wa nyuklia ni suala linalohitaji ushirikiano, ujuzi na uelewa wa pamoja. Kukutana kwa wataalamu kutoka nchi 18 hapa Arusha kunatoa nafasi ya kubadilishana uzoefu na maarifa ambayo yatasaidia kuimarisha uwezo wa nchi zetu katika kulinda nyenzo za nyuklia na vyanzo vingine vya mionzi,” amesema Ngamilo.
Ngamilo amesema TAEC itaendelea kutoa elimu na taarifa sahihi kwa umma kuhusu masuala ya usalama wa mionzi na nyuklia ili wananchi wawe na uelewa mpana kuhusu matumizi salama na yenye manufaa ya teknolojia ya nyuklia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akihitimisha hotuba yake, Prof. Najat ameishukuru IAEA kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kujenga uwezo wa kitaifa na kikanda katika usalama wa nyuklia, huku akiwataka washiriki kutumia kikamilifu siku tano za warsha hiyo kupata maarifa na uzoefu utakaosaidia kuleta maboresho katika nchi na taasisi wanazowakilisha.
Warsha hiyo inatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 9, 2026, jijini Arusha.










Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (Kulia), Akiwasalimia Wanachama wa Mfuko huo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma, Oktoba 5, 2026
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (Kulia), akimkabidhi cheti cha pongezi Afisa wa PSSSF, Bw. Dolphin Kaizer (katikati), kwa kutambua mchango wake katika kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa PSSSF, Bw. Hajji Khamis (kushoto). Cheti hicho amekabidhiwa leo Oktoba 5, 2026 wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma.Picha ya Pamoja ya Watumishi wa Mfuko wa PSSSF Makao Makuu Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Oktoba 5, 2026
Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa PSSSF, Bw. Hajji Khamis (kushoto) akimuhudumia mwanachama wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma, Oktoba 5, 2026.Afisa wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Jimmy Kamasho, Kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi mkoani Geita, akimuhudumia mwanachama wakati wa Wiki ya Huduma kwa wateja iliyoanza leo oktoba 5, 2026.
Dodoma, Oktoba 5, 2026
Katika hali inayoashiria upendo, kuwajali na kutambua mchango wa waajiri mbalimbali, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umejumuika na baadhi ya Waajiri katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 na kuwaomba waendelee kuwa mabalozi wazuri wa PSSSF katika maeneo yao ya kazi.
Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bw. Paul Kijazi alipokuwa akizindua Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo itaadhimishwa hadi Oktoba 9, 2026.
“Kwa namna ya kipekee napenda kutambua uwepo wa Waajiri mbalimbali na kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia katika maeneo mbalimbali katika kuhakikisha wanachama wa PSSSF wanapata huduma bora na kwa wakati. Na sisi tunaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi makubwa ya wanachama wetu, asanteni sana kwa kutuunga mkono.” Alisema Bw. Kijazi
Bw. Kijazi alisema, kauli mbiu ya mwaka huu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ni Hatua Moja Zaidi ( The Extra Mile), ambapo amewataka watumishi wa PSSSF kufanya yasiyowezekana yawezekane na wajue kwamba kutoa huduma bora kwa wanachama ni wajibu wao wa kwanza, na aliongeza, “Hivyo, tuendelee kusikiliza zaidi wanachama wetu, tuwe wa kwanza kuwafikia wanachama wetu, tutoe elimu sahihi na kwa wakati na tuendelee kutekeleza majukumu yetu kwa uadilifu kama kawaida yetu”.
Akizugumzia utoaji huduma kwa wanachama, alisema kuna watumishi wapo katika madawati ya huduma, hao ni pamoja na wenzetu wa kituo cha huduma kwa wanachama, Call Center na Kitengo cha Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, ambao mara nyingi ndio wa kwanza kukutana na wanachama wetu, aliwapongeza na kuwatia moyo waendelee kutoa huduma bora na aliwaomba watumishi wengine wawe tayari kuwasaidia pale wanapohitaji msaada wowote kwa lengo la kumhudumia vyema wanachama wa PSSSF.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Hajji Khamis alisema, “Tuwahudumie wanachama wetu kwa usawa, bila kujali nafasi zao, umri wao, eneo wanalotoka au aina ya huduma wanayohitaji. Siku zote tuzingatie muda wa huduma, usahihi wa taarifa,usiri wa taarifa za wateja na kufuata taratibu zetu tulizojiwekea ili tuweze kutoa huduma bora kwa wanachama wetu.
Mwisho
Na Mwandishi Wetu.
Rome, Italia. Tarehe 4 Oktoba 2026: Taasisi ya CRDB Bank Foundation imeendelea kujiimarisha kama daraja muhimu la mitaji ya kimataifa na jamii ambazo hazijafikiwa ipasavyo na huduma za fedha, baada ya kushiriki mkutano unaojadili Ufadhili Mseto wa Miradi yaani Blended Finance Working Group (BFWG) ulioandaliwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kujadili namna ya kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wananchi na biashara za vijijini.
Akishiriki mkutano huo uliowajumuisha wadau wengine ukiwamo Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Ujasiriamali ya Uholanzi (FMO), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), pamoja na wadau wa maendeleo, taasisi za fedha na wataalamu wa sekta mbalimbali, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema mikakati ya pamoja inahitajika kuwafikia wananchi wenye uhitaji wa mitaji nafuu ili nao washiriki kuujenga uchumi wa mataifa yao.
Serikali imesema Tanzania inakabiliwa na pengo la takribani dola bilioni 10 za Marekani katika fedha zinazohitajika kutekeleza mipango yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb), ameshiriki katika Tanzania Climate Finance Roundtable 2026, iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kimewakutanisha viongozi, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa mazingira, kwa ajili ya kujadili fursa na mikakati ya kuongeza upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Wizara ya Nishati ni mdau muhimu katika agenda ya tabianchi, hususan kupitia juhudi za kuongeza matumizi ya nishati safi, nishati jadidifu na teknolojia rafiki kwa mazingira, sambamba na kuimarisha usalama na upatikanaji wa nishati nchini.
































.jpeg)

.jpeg)
