Waziri wa Afya na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jenista Mhagama leo Aprili 15, 2025 amewasilisha ujumbe maalum kwa Ufalme wa Eswatini ambao umepokelewa na Waziri Mkuu wa Falme hiyo Mhe. Russell Mmiso Dlamini Jijini Mbabane, Eswatini.
Waziri Mhagama ameushukuru Ufalme wa Eswatini kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleza ushirikiano mzuri wa Kidiplomasia uliopo baina ya Mataifa hayo mawili.
Waziri Mhagama ameambatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji anayewakilisha Tanzania pia katika Falme ya Eswatini Bw. Ali Ubwa Mussa pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace, Magembe
Post A Comment: