NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk, Dotto Biteko ametoa rai kwa watanzaniakuendelea kudumisha amani na utulivu katika kuekea miaka 61 ya Muungano kwani Tanzania ili kuendelea kuwa nchi ya mfano Afrika kwa kudumisha Amani na mshikamano.
Naibu Waziri Dk, Biteko aliyasema hayo kijiji cha Esilalei Wilayani Monduli wakati wa ukaguzi wa mradi wa maji kwenye ziara yake ya siku nne anayoifanya wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha kuelekea Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Muungano.
Dk, Biteko alisema kunawatu wanasema maneno mengi kuhusu Rais Samia Hassan Suluhu lakini Rais haongei wala hawajibu badala yake anafanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wake
Alisema barabara, shule zinavyojengwa haziulizi dini, kabila wala vyama vya siasa na ni lazima watanzania wajue vinavyounganisha watu ni vingi kuliko vile vinavyowagawanya hivyo amani ni tunu pekee ya Taifa hili tuilinde.
Alisema anataka kuona Tanzania inabaki kuwa nchi ya mfano Afrika na Duniani kama nchi ya umoja yenye upendo inayohubiri amani kwaajili ya kujiletea maendeleo
Alisema Tanganyika na Zanzibar ziliungana tukapata nchi moja ya Tanzania kwani mataifa mengi yamejaribu kuungana yameshindwa na lakini Tanzania tumeunganishwa hivyo tupende mshikamano wetu .
Uchaguzi utakapofika chagueni kwa haki na angalieni mtu atakayewaletea maendeleo hata kama hajakupa soda mchague kwani anayekupa soda leo kesho hatakupa pia akiwa nyumbani kwake atasema hawa ndio wale niliowanunua lakini yule mliomchagua bila soda anajua kuwa anadeni kwa wananchi wake.
"Katika maisha haya tunayoishi utapimwa kwa kazi na si maneno hivyo tufanye kazi kwani watoto wenu na wajukuu zao watawaluliza mlifanya nini katika kuwaletea maendeleo, uchaguzi utakapofika chagueni mtu ambaye hata kama hajawapa soda mchagueni ili awaletee maendeleo "
Aliwasihi wanamonduli na wananchi wa Monduli kufanya kazi na kuleta maendeleo na kamwe wasigawanywe kwa misingi ya vyama na akitokea mtu anabeba dhana ya kusema badala ya kutenda akawapotosha na lazima watanzania wajue kuwa kusema ni rahisi lakini kutenda ni kugumu hivyo Rais Samia Hassan Suluhu anafanya kazi kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ikiwemo, maji, umeme, barabara na nk
Alisisitiza wananchi kufanya kazi zaidi na wasikubali kudanganywa na mtu yoyote kwa kabila, dini wala mahali walipotokea bali wote ni watanzania lakini kunavingi vinavyotuunganisha kuliko vinavyotaka kutugawanya lakini kunakundi linataka kututenganisha, tupendane na uchaguzi utakapofika chague mtu mwenye uwezo wa kuwaletea maendeleo.
"Mnanyemchagua bila soda yeye atajua anawaletea maendeleo na si yule anayewapa soda, lakini pia wafugaji jueni kuwa serikali yenu inawapenda zaidi"
Akizungumzia hukusu upatikanaji wa umeme katika wilaya hiyo Dk, Biteko alisema wilaya hiyo inajumla ya vijiji 62 ambavyo vyote vinaumeme na vitongoji 72 vimeshapelekewa umeme kati 236 huku vitongoji vingine vilivyobaki vikiendelea kusambaziwa umeme na baada ya uchaguzi mkuu kuisha umeme huo utafika katika vitongoji vingine
"Hizo nguzo 20 zilizopungua kuanzia kesho alhamisi hadi wiki ijayo nguzo hizo zitafika kijiji cha Esilalei ili wnaanchi wapate umeme na maendeleo"
Naye Naibu Waziri wa Madini, Dk, Stephen Kisurwa alisema uwepo wa mradi wa madini ya magadi soda wilayani Monduli utaapisha mapato ya halmashauri ya Monduli na kuongeza ajira ambapo kwa sasa halmashauri hiyo imekusanya kiasi cha sh, bilioni 3.6 badala ya sh,bilioni 5.7 kwa mwaka huu wa fedha
"Mradi huo wa magadi soda utakuwa na tija kubwa kwa nchi na wilaya ya Monduli utasaidia kupaisha mapato ya halmashauri hadi kufikia sh, bilioni 50 au bilioni 100 kwa mwaka kwasababu ya mradi huu wa magadi na utafungua barabara njia zaidi mawasiliano kama reli na barabara katika kuhakikisha madini hayo yanasafiri kwenda maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi"
Huku, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredy Lowassa alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuwaletea mradi huo wa maji lakini aliomba nguzo 20 za umeme katika kijiji cha Esilalei kwani vijiji 62 katika wilaya hiyo vinaumeme na vitongoji 72 kati ya 236 vimesambazwa umeme.
Awali, akisoma taarifa ya mradi huo Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) wilaya ya Monduli, Mhandisi Neville Msaki alisema mradi huo ambao umekamilika awamu ya kwanza utagharimu kiasi cha sh, bilioni 1.9 ambao utahudumia wananchi 8,757 kutoka vijiji vya Eslalei,Losirwa na makao mapya.
"Awamu ya kwanza ya mradi huu imeshakamilika na wananchi wa Eslalei na Losirwa wanapata maji na kuwapunguzia adha kina mama ya kutembea umbali wa kilomita 12 kufuata maji vijiji vya jirani lakini pia mifugo 26,400 itapata maji ya kunywa".
Post A Comment: