Na Denis Chambi , Tanga .

WATAALAMU wa Sheria wanaoenda kutekeleza kampeni ya msaada wa Kisheria 'Mama Samia legal Aid' Mkoani Tanga wametakiwa  kuhakikisha   wanawafikia wananchi wote mpaka ngazi ya mtaa  kutatua changamoto zao huku wakisisitizwa kuzingatia haki kwa kila mmoja.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tanga  Balozi Dkt Batilda Buriani Leo April 7 wakati akifungua mafunzo  ya kuwapa elimu watoa huduma ya msaada wa Kisheria watakwenda kuwahudumia wananchi mkoani hapa ambapo amesema kuwa uwepo wa timu hiyo utasaidia kupunguza malalamiko na kupunguza mashauri ambayo yamekuwa yakipelekwa katika ofisi mbalimbali ikiwemo Mahakamani.

"Nitoe wito kuhakikisha kuwa wananchi wote hususani wanyonge  wanafikiwa na kupata haki kwa wakati ,nyie kama wataalamu kwa nafasi mbalimbali mlizonazo zingatieni kufanya kazi kwa weledi na maadili ya kazi ili kuhakikisha kwamba mnakidhi haja na kiu za wananchi" 

"Naamini kuwa kwa pamoja tutasaidia kutatua kero ambazo saa nyingine viongozi wanakuja mabango yanakuwa ni mengi sana na sisi kwetu Tanga changamoto kubwa tuliyonayo ni migogoro ya ardhi, masuala ya Mirathi, ukatili wa kijinsia na watoto  limeanza kuwa ni donda ndugu ninaamini  kwa elimu ambavyo mtaipata hapa changamoto zitaendelea kupungua sana"  alisema Dkt Buriani.

Aida amewataka wataalamu hao kutumia nafasi zao vyema kwa kutoa elimu kwa wananchi katika kuzijua haki zao za msingi ili kuondokana na migogoro ambayo inaweza kuepukika.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa huduma za msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya katiba na sheria Ester Msambazi ameeleza kuwa mkoa  wa Tanga ambao ni wa 24  kupitiwa na kampeni hiyo tayari wameshaipata mikoa 23 ya Tanzania bara ambapo wamefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya  Milion 2.2

Alisema kampeni hiyo iliyoanza kutekelezwa April 2024 hadi sasa imekuwa na mafanikio makubwa hasa katika kuwahudumia wananchi kwa kutatua migogoro ya muda mrefu na kuwapatia haki ambapo ifikapo May 2025 inatarajia kutamatika rasmi ikiwa imefikia nchi mzima kwa upande wa Tanzania  bara na Zanzibar.

" Kampeni imekuwa na mafanikio makubwa sana tumeweza kufikia mtu mmoja mmoja katika mikoa 23 na kuwafikia watu zaidi ya Milion 2 na tumetatua migogoro mingi sana lengo ni kuhakikisha kwamba tunahimiza zaidi utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na tupunguze  mashauri Mahakamani" amesema Msambazi na kuongeza ...

"Kwa Mkoa wa Tanga tunatarajia kwamba kwa ile migogoro iliyodumu kwa muda mrefu timu yetu itaenda kutatua migogoro ile ili tuweze kukupunguza orodha ya wananchi wengi ambao wanafika  ofisini kwaajili ya kuwasilisha malalamiko"

Timu hiyo ya msaada wa Kisheria ya 'Mama Samia legal aid ' kutoka Wizara ya katiba na Sheria ambayo imeshapita katika mikoa 23 inashirikiana na wataalamu waliopo katika mikoa yote ambapo kwa Mkoa wa Tanga ifazifikia halmashauri 11 ikifanyika kwa siku 9.

Share To:

Post A Comment: