Na Denis Chambi, Tanga.
JUMLA ya wananchi 186 kati ya 3000 waliokwenda kupatiwa matibabu katika kambi maalumu ya macho wamefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa na tatizo hilo.
Matibabu hayo yanayotolewa bure na taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu kwa yameaanza April 5 hadi April 7, 2025 ambapo wananchi wengi wamegundulika kuwa na matatizo ya macho baada ya kufanyiwa uchunguzi ambapo wameweza kupatiwa Miwani na dawa ili kuweza kuwasaidia kuondokana na matatizo hayo.
Wakizungumza baadhi ya Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho Kibibi Swalehe, Morgan Kida pamoja na Sophia Abdallah wamewapongeza na kuwashukuru wadau wote walifanikisha kupatiwa matibabu ambayo wengi wamengeshindwa kuyapata kwa wakati kutokana na gharama kuwa kubwa
"Matibabu ya macho ni gharama kubwa kwa wananchi wa kawaida watu walikuwa wanatamani kutibiwa lakini watu walikuwa wanajiuliza na gharama, binafsi ni kwambasana jicho moja lilikuwa halioni kabisa nashukuru nmefanyiwa oparesheni ya mtoto wa jicho na sasa ninaiona bila shida yeyote nawashukuru sana kwa msaada huu waliotufanyia " amesema Morgan.
" Nashukuru sana kwa huduma hii tuliyoletewa na Bilal Muslim pamoja na mbunge wetu Ummy Mwalimu na huduma hii tungekuja moja kwa moja mpaka hospitali inhekuwa ni pesa nyingi lakini tumepata bure Mungu awabariki sana kwa msaada huu waliotufanyia" amesema Sophia.
Akizungumza mratibu wa kambi za macho kutoka taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Hassan Dinya amesema kuwa hadi zaidi ya wananchi 3,000 waliojitokeza wamepatiwa huduma wakati bado zo ezi likiendelea hii ikiongesha kuwa ikiongesha kuwa uhitaji ni mkubwa na wengi wanasumbuliwa na matatizo ya macho.
"Tumefikia hapa Mkoa wa Tanga kwaajili ya kuwachunguza wadonjwa na kuwafanyia matibabu bure na tangu juzi tumeweza kuwaona wagonjwa takriban 3,000 na kuwafanyia upasuaji wa macho wagonjwa 186 wagonjwa bado wagonjwa wana uhitaji mkubwa wa kufanyiwa matibabu tumejipanga kuhakikisha tunatoa huduma Bora ili wananchi tunaowahudumia waweze kuendelea na majukumu yao" alisema Dinya.
Akizungumza na wagonjwa hao Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha amewataka kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ikiwemo kutumia dawa walizopatiwa ili waweze kupona huku akiipongeza taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania na kuahidi ushirikiano baina yao na Serikali.
"Hii ni hatua nzuri ya kuunga juhudi za Serikali kupelekea huduma kwa wananchi Serikali tunaipongeza sana taasisi hii ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Kuna watu walikuwa hawana matumaini ya kupona lakini Leo hii tunaona watu wanaondoka kwa furaha kabisa niwaase sana wananchi hasa mliopata huduma hii mfuate ushauri wa wataalam ili waweze kupona kabisa na kwa haraka" alisisitiza Kubecha.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu amebainisha kuwa kuhudumia wananchi ni wajibu wa kila mmoja kulingana na uwezo aliojaliwa ambapo kupitia kambi hiyo wananchi wengi wengi waligundulika kuwa na changamoto ya macho wameweza kupata huduma.
"Kambi hii imerudiaha matumaini kwa wananchi wa Tanga kambi hii ni masuala ya maisha ya watu na sio siasa ukiwa na changamoto ya kipato halafu huoni inazidi kuwa masikini kwa sababu huwez kufanya chochote bila kuwa na msaidizi"
Ummy ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini hususani katika wilaya ya Tanga ambapo kupitia hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo idara ya macho imeweza kuboresha.
"Tunaishukuru sana Serikali yetu chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya mfano hapa katika hospitali yetu ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo sasa hivi kuna vifaa tiba vya kisasa wananchi wanaendelea kupata huduma , taasisi ya Bilal Muslim tunaishukuru sana imesaidia wananchi wengi kutokupata upofu wa macho" amesema Mbunge huyo.
Post A Comment: