KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya,akipanda Mti kuonesha uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti inayokwenda kwa jina la Mti Pesa katika Shule ya Msingi Mtumba iliyoratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) .

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya,akiumwangia Maji Mti alioupanda wakati akizindua kampeni ya upandaji miti inayokwenda kwa jina la Mti Pesa katika Shule ya Msingi Mtumba iliyoratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) .

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya,akimpongeza Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) Bi. Fikira Ntomola,wakati akipanda Miti katika Shule ya Msingi Mtumba jijini Dodoma iliyoratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) .

Wanafunzi Shule ya Msingi Mtumba jijini Dodoma wakipanda Miti.

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya,akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kampeni ya upandaji miti inayokwenda kwa jina la Mti Pesa katika Shule ya Msingi Mtumba jijini Dodoma iliyoratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) .

Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) Bi. Fikira Ntomola,akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya upandaji miti inayokwenda kwa jina la Mti Pesa katika Shule ya Msingi Mtumba jijini Dodoma iliyoratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) .

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya,akigawa vitabu vya elimu ya fedha kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuzindua club za Fedha Mashuleni.

Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) Bi. Fikira Ntomola,akiwa na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtumba wakiwa wameshikilia Vitabu mara baada ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya (hayupo pichani) kuzindua club za Fedha Mashuleni.

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua kampeni ya upandaji miti inayokwenda kwa jina la Mti Pesa katika Shule ya Msingi Mtumba jijini Dodoma iliyoratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) .

Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya, amezindua kampeni ya upandaji miti inayokwenda kwa jina la Mti Pesa ililofanyika katika maeneo ya wazi ya shule ya msingi Mtumba iliyoratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) ambayo imeenda sambamba na Uzinduzi club za Fedha Mashuleni.
Akizungumza leo Aprili 11,2025 jijini Dodoma mara baada ya kuzindua kampeni hiyo Bw.Mmuya amesema kuwa jumla ya miti ya matunda 2000 inatarajiwa kupandwa katika Shule 4 za Msingi zilizopo katika Mkoa wa Dodoma ambapo miti 500 ya matunda iliyotolewa na Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha (TAWIFA) imepandwa katika Shule ya Msingi Mtumba Jijini Dodoma.
Bw.Mmuya amesema lengo la kupanda miti hiyo ya Matunda mashuleni ni pamoja na kuwafundisha watoto kuwa chanzo cha mapato kinaweza kupatikana hata kwa kupanda miti hasa miti ya matunda.
"Kwa Wastani kipato cha mtu mmoja mmoja Dodoma hakizidi milioni 2 kwa mwaka, kwahiyo tukasema kwa kupanda miti ya matunda tunategemea kiwe ni chanzo kikubwa cha familia na mtu mmoja mmoja kukuza kipato,kwahiyo tumeanza na shule tano ikiwemo hii ya Mtumba kwa kupanda miti 500 lakini kwa zote 5 tutapanda miti 2000 lengo likiwa ni kufundisha watoto kuwa chanzo cha mapato kinaweza kupatikana hata kwa kupanda miti hususan ya Matunda".amesema Bw.Mmuya
Amesema katika shule hizo nne, itapandwa miti 2,000 kwa mgawanyo wa miti 500 kila shule, huku lengo ni kuwafundisha watoto kuwa mapato yanawezekana kupatikana kwa kupanda miti ya matunda.
Hata hivyo amesema katika kipindi cha kati ya mwaka 2017, kampeni ya kukijanaisha Mkoa wa Dodoma, imeweza kupanda miti milioni 16.
Aidha, amesema wametenga bajeti katika halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya upandaji wa miti kupitia programu ya ‘mti wangu birthday yangu’.
Amesema kila halmashauri imepanga bajeti isiyopungua Sh10 milioni kwa ajili ya upandaji na utunzaji wa miti hususani ya matunda katika mwaka 2025/26.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) Bi. Fikira Ntomola amesema kuwa wao wanataka kuonesha kuwa kupanda miti sio kwa ajili ya kutunza Mazingira tu bali hata katika katika kuchochea uchumi wa Nchi kwa kuhamasisha kupanda miti ya Matunda kama wao wanavyofanya katika Kampeni yao.
"TAWIFA inazundua Kampeni kubwa inayoitwa mti pesa na imekuja na Kampeni hii kwaajili ya kusukuma zaidi ajenda ya kukijanisha Dodoma lakini kukabailiana na mabadiliko ya tabia ya nchi na hali ya hewa kwa ujmla tukianza na Mkoa wa Dodoma ambapo pia tunataka kuonesha kuwa kupanda miti sio kwaajili ya kutunza Mazingira tu lakini pia inachochea uchumi wa nchi yetu "amesema
Aidha amesema kwa kupanda miti hiyo,kunamjenga mwanafunzi kujiwekea dhamira kuwa hakuna kitu kinachokuja kirahisi bila kufanya kazi.
Amesema shughuli ya upandaji miti, itafuatiwa na utoaji wa elimu ya fedha kwa wanawake wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma na mkutano mkuu wa mwaka.
Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Mtumba Mwl.Kepha kitutu amemuhakikishia Katibu Tawala utunzwaji wa miti hiyo kwani itasaidia shule hiyo katika kutunza mazingira, kuwapatia vivuli na wanafunzi kujipatia chakula chenye lishe.
Share To:

Post A Comment: