Na Denis Chambi, Tanga.
WADAU wa usafirishaji kwa njia ya maji hapa nchini wametakiwa kufuata Sheria na kanuni zinazosimia sekta hiyo ikiwemo kutekeleza matakwa ya leseni walizopewa pamoja na kuzingatia weledi na ufanisi wakati wa utoaji wa huduma bandarini.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa kudhibiti huduma za usafiri kutoka shirika la uwakala wa Meli Tanzania 'TASAC' Nelson Mlali Mkoani Tanga wakati wa kikao cha pamoja na wadau wa usafiri kwa njia ya maji kilichoandaliwa na kwa lengo la kutoa elimu na kukumbushana wajibu wao katika kutekeleza huduma hiyo kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za nchi.
Mlali amesema kwa kutofuata Sheria na taratibu za utoaji wa huduma kwa wadau hao kutashusha kiwango cha ufanisi AA bandari zilizopo hapa nchini na kuifanya kuingia kwenye ushindani na nchi nyingine hali ambayo inaweza kupelekea wafanyabiashara kwenda kufanya kazi nje.
"Lengo letu kubwa ni kukaa nao tuone ni maeneo gani ambayo hayafanyi vizuri ili waweze kufanya vizuri kwaajili ya faida ya bandari zetu hapa nchini tungependa pia tupunguze malalamiko, migogoro na ucheleweshwaji wa utoaji huduma za usafiri kwa njia ya maji"
"Tunapochelewesha utoaji wa huduma kwa uzembe au kwa kutokuju kunazifanya bandari zetu kukosa wateja na wao wenyewe kama wafanyabiashara wanapoteza kazi nyingi zinakuwa haziji upande wetu zinaenda katika mataifa shindani" amesema Mlali.
"Changamoto iliyopo kwa hawa tunaowasimamia ni kutokufauta utaratibu na Sheria baadhi yao , ucheleweshwaji wa huduma na kuwepo kwa malalamiko yanayotokana na shughuli zao za utoaji wa huduma wito wangu kwao watoe ushirikiano ili tuweze kupunguza uwepo wa malalamiko na hatimaye tuweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi katika mnyororo mzima wa usafirishaji wa bidhaa kwa njia ya maji" aliongeza.
Kwa upande wake Afisa mfawidhii kutoka shirika la uwakala wa' Meli Tanzania 'TASAC' mkoa wa Tanga Christopher Shalua amewataka wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji kuhakikisha kupitia sekta zao za afya wanazingatia usalama kabla na baada ya kutoa huduma za kupakuwa na kupakia mizigo kweli Meli hususani zinazotoka nje ya nchi.
"Eneo la bandari ni eneo ambalo Lina mashara mengi kuna taasisi ambazo zinafanya kazi zao bila kujua kwamba wanaweza wakaingiza magonjwa hapa nchini Kuna baadhi ya takataka zianzokuja kwetu kwa njia ya Meli zinazotoka nje watu wa sekta ya afya lazima wahakikishe kwa nafasi zao hakuna madhara yanayotokea kwenye nchi yetu kupitia vyombo tunavyohudumia" alisisitiza Shalua.
Aidha afisa huyo amewataka wadau wote wa usafirishaji kwa jia ya maji kuhakikisha wanafuata Sheria na taratibu za nchi ikiwemo kuhusiaha lwseni zao ili waweze kupata ruhusa ya kufanya kazi zao bandarini wakati wote.
"Mawakala na wadau wote wanaotoa huduma za bandari lazima kuhakikisha kuwa vibali vyao vinahuishwa ili kufuata taratibu na Sheria za nchi yetu katika utoaji wa huduma bandarini" ameongeza
Kwa upande wao wadau walioshiriki kikao kikao kazi hicho akiwemo Amri Sufiani pamoja Happiness Kayange wameipongeza shirika la uwakala wa' Meli Tanzania 'TASAC' kwa kuendelea kuwapa elimu na kuwakubusha wajibu wao sambamba na kuboresha utoaji wa huduma kwa maslahi ya Taifa.
"Tunawapongeza sana TASAC kwa kuona umuhimu wa kutupatia elimu hii ambayo imetusaidia kutekeleza majukumu yetu katika kuwahudumia wateja jambo hili ni zuri kwa sababu Kila mdau anajua wajibu wetu katika kuwahudumia wateja wanapofika kwetu" alisema Sufiani.
Tunawashukuru sana TASAC kwa kutuweka pamoja ambapo kupitia elimu wanayotupa inatusaidia kutekeleza na kuzijua Sheria ili kufanya kazi kwa viwango Bora vinavyotakiwa , wamwtusaidia pia kuwajua wadau wengine ambao tunaweza kufanya nao kazi kwa maslahi ya nchi yetu" alisema Happiness.
Post A Comment: