Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dk Jacqueline Mkindi.
TAASISI kilele ya Kilimo cha Horticulture Tanzania (TAHA) imetangaza mkakati wa kufungua soko la mboga na matunda la Italia lenye thamani ya dola bilioni 19 kwa mwaka.
TAHA itapeleka wafanyabiashara wakuu wa mazao ya horticulture kwenye ziara ya kibiashara nchini Italia, kwa ushirikiano na Wakala wa Biashara wa Italia (ITA), ili kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Macfrut kuanzia Mei 4 hadi 9, 2025.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dk. Jacqueline Mkindi, alisema ziara hiyo inalenga kufungua fursa mpya za kibiashara, kuimarisha ushirikiano, na kuungana na wanunuzi wa kimataifa.
Wafanyabiashara wa Kitanzania watashiriki katika mikutano ya kibiashara na kongamano la soko la horticulture, linalotoa mtizamo wa kina kuhusu fursa za Italia.
TAHA ina historia ya mafanikio, ikiwa imesaini mikataba ya dola milioni 12.6 katika Maonyesho ya Fruit Logistica 2025 nchini Ujerumani.
Italia, ikiwa mwaagizaji wa saba wa mboga duniani, inatoa fursa kubwa kwa Tanzania, ambayo mauzo yake ya sasa nchini humo ni madogo (dola elfu 45.5 mwaka 2022).
Takwimu zinaonyesha Italia inaagiza mboga za thamani ya dola bilioni 19.3, hasa kutoka Uhispania, Uholanzi, Ufaransa, Brazili, na Ujerumani.
Mkakati wa TAHA unajumuisha mafunzo yaliyoandaliwa na ITA Februari 2025, yaliyolenga kuimarisha ujuzi wa wajasiriamali wa Kitanzania kwa soko la Ulaya.
Kampuni zilizoshiriki mafunzo hayo zitashiriki katika ziara ya Mei, ikiwa na lengo la kuimarisha mnyororo wa thamani, kukuza ushirikiano na Italia, na kuongeza ajira na fedha za kigeni nchini Tanzania.
Dk. Mkindi alisisitiza kuwa hii ni hatua ya kimkakati ya kuimarisha nafasi ya Tanzania katika soko la kimataifa la horticulture, akiongeza kuwa fursa za tasnia hii nchini hazina mipaka
Post A Comment: