Baraza la Wafanyakazi la Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) limekutana na kufanya kikao kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yatakayosaidia kurahisisha utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi pamoja na kukabidhi mkataba wa kuunda Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathimini wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Daudi Mayeji aliyemwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema uwepo wa meli tatu za uvuvi zenye uwezo wa kuvua kwenye bahari kuu utalisaidia shirika la uvuvi nchini TAFICO kujiendesha lenyewe kwa kujiingizia kipato kupitia uvuvi badala ya kuendelea kuitegemea Serikali.
Pia amesema baraza la wafanyakazi siyo tu jukwaa la majadiliano bali ni daraja linalounganisha wafanyakazi na waajiri hivyo ni chombo kinachowezesha wafanyakazi kutoa mawazoyao juu ya maendeleo ya shirika, kutoa mapendekezo juu ya mazingira ya kazi pamoja na kushiriki katika mchakatowa kufanya maamuzi yanayogusa maisha yao.
Mayeji ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi mkataba wa kuunda baraza la wafanyakazi la TAFICO lenye lengo la kuweka mazingira ya uwazi na kusikiliza mawazo ya wafanyakazi ndani ya taasisi hiyo
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Ahmed Byabato amesema kufanyika kwa vikao hivyo vya Baraza ni kuimarisha demokrasia mahala pa kazi,na kuwataka wajumbe wa Baraza hilo kurudisha mrejesho kwa watumishi wenzao na kuwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kutenda kazi kwa ufanisi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Daudi Mayeji aliyemwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi pamoja na kukabidhi mkataba wa kuunda Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Ahmed Byabato akizungumza na wajumbe wa Baraza pamoja na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Daudi Mayeji aliyemwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa ufunguzi wa Baraza la Shirika hilo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Daudi Mayeji (kushoto) akimkabidhi mkataba wa kuunda Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kaimu Mtendaji Mkuu wa TAFICO Ahmed Byabato .
Baadhi ya wajumbe wa baraza pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji iliyosomwa na Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Daudi Mayeji wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi pamoja na kukabidhi mkataba wa kuunda Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Picha ya pamoja
Post A Comment: