Na Denis Chambi ,Tanga
SPIKA wa baraza la wawakilishi
Zanzibar Zuberi Maulidi ameawataka watanzania kuendelea kuenzi na kudumisha
tunu ya muungano kati ya Tanganyika na
Zanzibar iliyoasisiwa miaka 61 iliyopita kwa kuhakikisha kuwa amani na umoja vinaendelea kutawala kwa
kuweka maslahi ya Taifa mbele.
Spika Maulidi ametoa wito huo mkoani Tanga katika maadhimisho ya muungano ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Aprili 26 ambayo mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo ‘Muungano wetu ni dhamana heshima na tunu ya taifa shiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 akisistiza watanzania wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwa upande wa udiwani ubunge na kiti cha Rais.
Adha ameataka watanzanai waliopewa dhamana ya kusimamaia sekta mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwa wanatekeleza vyema majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamaia maono ya serikali kawenye miradi ya maendeleo.
Awali akizungumza mkuu
wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani tangu kuasisisiwa kwa muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kupitia awamu zote ni mambo mengi ya kimaendeleo
yamefanyika hususani kwenye awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhri ya muungano
wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Tanga amabaye ni naibu waziri wa maliasili na utalii Datan Kitandula amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt SAmia Suluhu Hassan kupitia sekta mbalimbali ikiwmo afya ,elimu, miundombinu ambapo mkoa huo umenufaika kwa miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati.
“Kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Tanga tunampongeza sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika muda ambao tumekuwa wawakilishi wa wananchi hatukuwahi kuona maendeleo makubwa kama haya ya kipindi cha awamu ya sita anayoiongoza” amesema Kitandula
Post A Comment: