Kampuni ya Shree International Tanzania Limited imeahidi kuchangia ujenzi wa chumba kimoja cha upasuaji na gari moja la kuhudumia wagonjwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Mkurugenzi Mtendaji wa Shree International Tanzania Limited, Bw. Jadgish Naran Vekariya ametoa ahadi hiyo leo Jumatano Aprili 16, 2025 wakati wa kikao kazi kati ya Kampuni hiyo na MOI.

Bw. Jagdish amesema kwamba kampuni yao itachangia ujenzi wa chumba kimoja  cha upasuaji na gari moja la wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitiahada za taaisi hiyo katika kutoa tiba bora.

"Kama kampuni tutachangia gharama ya ujenzi wa chumba kimoja cha upasuaji na gari moja kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa hapa MOI, tumeamua kusaidia matibabu ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambao hawana uwezo ili kurejesha nguvu kazi kwa Taifa" amesema Bw. Jagdish na kuongeza kuwa 

“Tumekuwa tukitoa msaada wa gharama za matibabu hapa MOI kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo hadi sasa jumla ya Tsh. 26 miliomi tumesaidia watoto hao wanaotibiwa hapa MOI”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya ameishukuru kampuni hiyo kwa kuthamini na kujali watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi kwa kuchangia gharama za matibabu na kutoa ahadi ya kuchangia ujenzi wa chumba kimoja cha upasuaji pamoja na gari la wagonjwa.

"Niwashukuru kwa mchango wenu mkubwa katika kusaidia kuchangia gharama za matibabu kwa watoto wenye changamoto ya kichwa kikubwa na mgongo wazi, msaada huu ni muhimu katika kujenga nguvu kazi kwa Taifa letu pale tunapoona watoto hawa wanarejea nyumbani baada ya matibabu yao kukamilika" amesema Dkt. Mpoki na kuongezea

"Kama taasisi tupo katika mchakato wa kupanua sehemu zetu za vyumba vya upasuaji, kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa haswa wanaosababishwa na ajali za barabarani na tungependa tushirikiane nanyi ili kufanikisha mpango huo"










Share To:

Post A Comment: