Na. Peter Haule, WF, Dodoma.
Serikali imesema kuwa ina mpango wa kujenga vituo sita vya forodha mipakani katika mwaka wa fedha ujao wa 2025/26.
Hayo yalisema bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Oliver Daniel Semuguruka, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuanza ujenzi wa Kituo cha Forodha katika Kijiji cha Mukikoro, Kata ya Mugoma - Ngara.
Mhe. Chande alisema kuwa Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 1.1 ya ujenzi wa vituo Sita vya forodha kikiwemo kituo cha forodha Mugoma kilichopo Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Burundi kwa mwaka ujao wa fedha
Post A Comment: