Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan itaendelea kuratibu shughuli za UKIMWI kwa kutoa huduma endelevu na stahimilivu kwa WAVIU, kuimarisha Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI ili uweze kufanikisha malengo ya nchi katika kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030

Hayo yamesemwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa  wakati akiwasilisha hotuba yake kuhusu mapitio na kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2025/2026

Amesema sambamba na hayo, Serikali inatambua mabadiliko ya kisera kutoka kwa baadhi ya washirika wetu wa muda mrefu wa masuala ya UKIMWI. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali inachukua hatua madhubuti kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha uwekezaji kwenye eneo la utaoji huduma kwa WAVIU

Aidha kwa mujibu wa takwimu zilizopo, watu 1,536,842 kati ya watu 1,690,948 wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi. Kadhalika, WAVIU 1,545,880 wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU ambapo watu wazima wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ni asilimia 96.4.

Share To:

Post A Comment: