Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili, 2025.
Katika mazungumzo yao Rais Dkt. Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibitimuingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Kupitia Taasisi yake ya Six Rivers, Sir Jim Ratcliffeamebainisha kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhiya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha pamoja na Jezi ya Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) yenye Ujumbe wa, “Amaizing Tanzania” kwa Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza iliyosainiwa na Wachezaji wa Timu hiyo kutoka kwa Mmiliki wa Klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili, 2025. Mmiliki wa Klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe ameeleza dhamira yake ya kuitumia Klabu yake kutangaza utalii nchini Tanzania. Rais Dkt. Samia pia amemkaribisha Mmiliki huyo wa Club ya Manchester kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini.
Post A Comment: