MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF umetoa elimu ya Hifadhi ya Jamii na utekelezaji wa shughuli za Mfuko tangu ulipoanzishwa mwaka 2018, mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaofanyika kwenye Ukumbi wa Parokia ya Familia Takatifu Bombambili Kanisa Katoliki jimbo Kuu Songea, mkoani Ruvuma Aprili 4, 2025.
Akitoa mada mbele ya wajumbe hao, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, Bw. Yesaya Mwakifulefule, alisema, Mfuko umekuwa ukitekeleza majukumu yake ipasavyo ya Kusajili Wanachama, Kukusanya Michango, Kulipa Mafao na Kuwekeza.
“ Thamani ya Mfuko wa PSSSF imefikia trilioni 10, haya ni mafanikio makubwa ya Mfuko tangu ulipoanzishwa mwaka 2018.” Amesisitiza Bw. Mwakifulefule.
Aidha, Mfuko unajivunia kufanya mapinduzi makubwa katika utioaji wa huduma zake, ambapo kwa sasa umeqachana na matumizi ya karatasi katika kuwahudumia wanachama na badala yake huduma zote zinatolewa kupitia mtandao maarufu PSSSF Kidijitali, alisema.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile, amepongeza taasisi zilizosaidia kuwezesha kufanyika kwa mkutano huo ambapo PSSSF imepewa tuzo ya shukrani kwa kuwa miongoni mwa taasisi hizo.
Post A Comment: