
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Dkt. Ladislaus Chang’a (kushoto) wakionyesha hati za makubaliano mara baada ya kusaini Machi 31,2025 jijini Arusha.
.....
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ( NM-AIST) imesaini makubaliano ya ushirikiano na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika masuala ya utafiti na sayansi kwenye maeneo mbalimbali yanayohusu mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi, ikiwemo namna mabadiliko hayo yanavyoathiri afya ya akili kwa kushirikisha Chuo Kikuu cha Hurbert Kairuki.
Hayo yamesemwa Machi 31, 2025 jijini Arusha na Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula ambaye ni Mwenyeji wa Warsha ya Jopo la Kimataifa la Sayansi na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia ya Nchi kwa uratibu wa Kituo cha Umahiri cha WISE-Future kwa kushirikiana na TMA.
Alieleza kuwa, NM-AIST na TMA imekubaliana kushirikiana katika maeneo makuu matatu ikiwemo utafiti katika masuala ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia ya nchi, kuwajengea uwezo wataalamu wa TMA kupitia mafunzo ya muda mfupi pamoja na kuendeleza Teknolojia na Ubunifu, kupitia matumizi ya teknolojia kidigitali ikiwemo Akili Mnemba ( AI).
“Sisi kama Taasisi ya kikanda tunafurahi sana kuwa sehemu ya tukio hili , ambalo limetupa fursa ya kutoa mchango wetu kwenye taarifa ya tathmini ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia ya nchi duniani” Prof. Maulilio Kipanyula.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya Hewa Nchini (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a,ametoa wito kwa wananchi kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka hiyo hususani tahadhari ya hali mbaya ya hewa.
“Mambo makubwa yaliyofanyika hapa ni kuhakikisha wataalamu kutoka Tanzania, Afrika na ukanda wa nchi zinazoendelea wanashiriki kwa wingi katika kazi za kisayansi katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi” alisema Dkt. Ladislaus Chang'a Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Dkt. Chang'a alisema kuwa, makubaliano ya ushirikiano na NM-AIST ni kuchagiza na kuongeza ufanisi na tija katika huduma za hali ya hewa kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa ikiwemo akili mnemba ,Sayansi, Teknolojia na ubunifu.
Warsha ya Jopo la Kimataiafa la Sayansi na mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia ya Nchi , imeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shahada ya uzamili na uzamivu katika masuala ya mazingira na biolojia, Msalaba Mwekundu na NEMC.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini,Dkt. Ladislaus Chang’a (kushoto) wakionyesha hati za makubaliano mara baada ya kusaini Machi 31,2025 jijini Arusha.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Dkt. Ladislaus Chang’a (kushoto) wakisaini makubaliano ya mashirikiano Machi 31,2025 jijini Arusha.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) akipokea Jarida la Tathmini ya Hali ya Hewa Nchini kwa Mwaka 2024.0 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Prof. Jaji Mshibe Ali Bakari ( Kulia ) katika Warsha ya Jopo la Kimataifa la Sayansi na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia ya Nchi Machi 31,2025.
Wadau waliohudhuria Warsha ya Jopo la Kimataifa la Sayansi na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na tabia ya nchi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa na Wataalam Machi 31,2025 Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Prof Jaji Mshibe Ali Bakari ( katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakati wa Warsha ya Jopo la Kimataifa la Sayansi na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na tabia ya nchi Machi 31,2025.
Post A Comment: