Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka watanzania kujenga Taifa lenye Mshikamano, Amani na Umoja kama ambavyo Muasisi wa Taifa Mwalimu JK, Nyerere alivyofanya katika kuwajenga watanzania.
Mhe. Biteko ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua Kongamano la kumbukizi la kuzaliwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), katika ukumbi wa Utamaduni kampasi ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Biteko amesema kumbukizi ya kongamano Hilo linatoa fursa kwa Watanzania kukutana na kutafakari kwa pamoja katika kujenga Taifa lenye mshikamano ambapo Baba wa Taifa alisisitiza misingi ya kuunganisha Makabila yote bila kujali kuangalia kwa kutuunganisha makabila yote bila kujali dini, na rangi ya mtu na kuwa kitu kimoja kwa lengo la kuleta Maendeleo katika.
Mhe. Biteko amewataka vijana wa kitanzania kufanya tafakuri ya mambo ambayo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu JK. Nyerere aliyaamini na kuyaishi kwa kujifunza kupitia makongamano ya aina hii ili kudumisha Amani, Upendo na Umoja wa kitaifa.
Akimkaribisha Mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara na Mwenyekiti wa bodi ya MNMA Mhe. Stephen Wasira amesema Mwalimu Nyerere amewaunganisha Watanzania wote bila kujali dini wala kabila na kuwa kitu kimoja pia ameliacha Taifa likiwa na Amani hivyo Amani hiyo inatakiwa kulindwa kwa nguvu na kutoruhusu watu ama kikundi chochote kuvuruga Amani aliyotuachia Muasisi wa Taifa Mwalimu JK. Nyerere.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Haruni Mapesa amesema lengo la Kongamano la Kumbukizi ya kuzaliwa Mwalimu JK.Nyerere ni kuyaenzi, kutafakari na kuyazungumzia kwa pamoja juu ya Fikra, Mawazo na Itikadi zake hasa kupitia mada kuu isemayo Maono ya Baba wa Taifa Mwalimu JK. Nyerere katika Elimu, Uwekezaji, na Ujenzi wa Taifa lenye Amani kwa Maendeleo ya Watu.
Prof. Mapesa ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Kukipatia Ruzuku ambazo zinasaidia katika Kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Chuo.
Kongamano la kumbukizi la kuzaliwa Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere huandaliwa na Chuo kila mwaka kwa lengo la kuenzi na kutafakari Falsafa na Maono ya Baba wa Taifa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
11.04.2025
Post A Comment: