Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Ndugu Abdulhabib Mwanyemba amekabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi Kwa ajili ya muendelezo wa Nyumba za UVCCM Wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Dodoma.
Vifaa hivi ni sehemu ya Utekelezaji wa Ahadi aliyoitoa Mwenyekiti pamoja na kamati ya Utekelezaji Mkoa katika ziara yao waliyoifanya Mkoa mzima juu ya kuzisaidia Wilaya kufanikisha Juhudi zao za kukamilisha nyumba hizi kupitia mchango wa vifaa vya Ujenzi.
Wilaya ambazo zimekabidhiwa vifaa vya ujenzi Kwa awamu ya kwanza ni Mpwapwa, Kongwa, Chamwino na Bahi. Kila Wilaya imepewa vifaa vyenye thamani ya Tsh 500,000 kupitia mapato ya ndani ya Mkoa. Mwenyekiti ameahidi kuendelea na utaratibu huu wa Mkoa kuzipa nguvu Wilaya zilizobaki na kutoa motisha zaidi Kwa Wilaya itakayoonyesha Juhudi katika kukamilisha ujenzi.
Imetolewa na
Wenceslaus Mazanda
Katibu wa Uhamasishaji na chipukizi Mkoa
Dodoma
Post A Comment: