Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme amesema zipo fursa nyingi ambazo Taifa hunufaika kwa kuwa wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD).

Ameyasema hayo Dodoma Aprili 16, 2025 wakati akifungua Kikao cha UNCCD ambapo ameeleza fursa hizo ni pamoja na kujengewa uwezo wa kitaalam, kifedha na kupatiwa vitendea kazi kwaajili ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.

Katika Mkataba huu, Ofisi ya Makamu wa Rais ndio Ofisi Kiungo ya Kitaifa (National Focal Point) kati ya Serikali na Sekretarieti ya Mkataba. Katika kutekeleza majukumu chini ya Mkataba huu, nchi mwanachama pamoja na masuala mengine.

“Kwa kuwa mwanachama, Jamuhuri ya MuunganoTanzania imeweza kunufaika na fedha kutoka katika mifuko mbalimbali ya kimataifa ya Kimazingira kama vile GEF, GCF, LDCF, AF na nyinginezo,” amesema Bi. Mndeme.

Amesema Mifuko hii imeweza kutupatia fedha kwa ajli ya kutekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi (Sustatinable Land Management - SLM) na hivyo kupunguza kuenea kwa hali ya jangwa na Ukame katika maeneo yaliyo athirika na changamoto hii.

Kwa upande wake Afisa Kiungo wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD) Bw. Thimotheo Mande amesema kuwa mwanachama wa Mkataba huu Serikali pia kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeweza kufanya Tafiti mbalimbali na kuandaa taarifa ambazo zinatoa uelekeo.

Amesema Disemba, 2024 ulifanyika Mkutano wa kumi na sita wa nchi wanachama wa UNCCD, Mkutano huu ulifanyika Jijini Riyadh Saudi Arabia ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilishiriki.

Ushiriki wa Tanzania uliratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Khamis H. Khamis akiambatana na viongozi mbalimbali kutoka OMR pamoja na Wataalam mbalimbali.







Share To:

Post A Comment: