Mwenge wa Uhuru umepitia miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 1.197, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera za Serikali ya Awamu ya Sita.

Kati ya miradi hiyo, mitatu imezinduliwa, mmoja umewekewa jiwe la msingi, na mingine mitatu imekaguliwa.

Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Kibaha, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,  Petro Magoti Itozya, ameeleza kuwa kati ya fedha hizo, sh. milioni 599.3 zimetolewa na Serikali Kuu, na mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ni sh.milioni 178.1.

Magoti ameongeza kwamba wahisani wamechangia sh.milioni 409.6, wananchi wakichangia nguvu zao za maendeleo kiasi cha sh.milioni 4.750, huku michango ya Mwenge ikiwa ni sh.milioni 5.6.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi, ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, akieleza kuwa ni wazi miradi hiyo itachochea maendeleo ya Wilaya ya Kisarawe na kuleta manufaa kwa wananchi.

April 4 mwaka huu Mwenge wa Uhuru utapokelewa wilayani Mkuranga. 





Share To:

Post A Comment: