Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema mfumuko wa bei kwa mwaka 2024 umepungua hadi kufikia wastani wa asilimia 3.1 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.8 mwaka 2023.
Amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba yake kuhusu mapitio na muelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2025/2026
Aidha amesisitiza kuwa Kiwango hicho kipo ndani ya lengo la nchi na Jumuiya za kikanda la wigo wa asilimia 3.0 hadi 5.0 katika muda wa kati. Kupungua kwa mfumuko wa bei kulitokana na utekelezaji wa sera madhubuti za fedha na bajeti; uwepo wa utoshelevu wa chakula nchini; na uboreshaji wa miundombinu ya uchukuzi iliyorahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka maeneo ya uzalishaji hadi kwenye masoko.
Post A Comment: