Na Denis Chambi, Tanga.
TAASISI ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Leo April 5,2025 imeanza zoezi la matibabu ya macho Bure kwa wananchi wa halmashauri ya Jiji la Tanga ikiwa ni katika jitihada za kukabiliana na matatizo mbalimbali ya macho ikiwemo mtoto wa jicho ambapo tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wananchi Mkoani Tanga wamemeathirika na tatizo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu amesema kuwa taasisi hiyo ambayo inafanya kambi hiyo kwa mara ya pili jijini hapa kutoka ile ya mwaka 2019 ambapo zaidi ya wananchi 3,000 waligundulika na tatizo la mtoto wa jicho na walipatiwa matababu, dawa pamoja na Miwani bure.
"Wadau wetu kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania wanakuja tena Tanga kwaajili ya kuiendesha kambi hii kubwa ya macho bure tulifanya mwaka 2019 niliwaomba na nashukuru Wamekubali ombi letu la kuja kutoa huduma hii kwa siku tatu kuanzia jumamosi hadi jumatatu katika viwanja vya shule ya Sekondari Usagara"
"Huduma zitakazotolewa katika kambi hii kubwa ni kupima na kupewa Miwani bure, watu wana kumbukumbu 2019 tulitoa Miwani zaidi ya elfu tatu kwa wakazi wa Jiji la Tanga ambao walipimwa na kukutwa na changamoto za macho"
"Lakini kambi hii itatoa dawa bure kwa watu ambao watapimwa na kukutwa na changamoto za macho na kutoa ushauri wa afya ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa wa macho na pia itatoa huduma za kusafisha mtoto wa jicho nure kabisa" alisema Ummy
Aidha mbunge huyo ameipongeza na kumshukuru taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Kwa utayari wao wa kuendeleza ushirikiano ili kuwasaidia wananchi Kwa kushirikiana na ofisi ya mganga Mkuu wa wilaya hiyo kupitia kambi hiyo ambayo imedhaminiwa na kampuni ya simu za Mkononi ya Yas.
"Napenda sana kuwaalika wakazi wote wa wilaya ya Tanga kujitokeza kwa wingi kuanzia saa mbili asubuhi mpaka sasa tisa na nusu, naomba watu wafike mapema wapewe huduma " alisisitiza Mbunge huyo.
"Mimi kama mbunge wa Jimbo la Tanga niwashukuru sana Bilal Muslim Mission of Tanzania Kwa kukubali ombi letu kuja kufanya kambi hii bure lakini jambo hili tunashiriana na ofisi ya mganga ya wilaya ya Tanga chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Yas" alisema Ummy.
Akizungumzia kambi hiyo Dkt. Hussein Abas kutoka taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania ambaye ni daktari bingwa wa macho na mratibu wa macho kwa Mkoa wa Tanga amebainisha kuwa tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wananchi Mkoani hapa wana shida ya mtoto wa jicho.
Dkt Hussein ameongeza kuwa wamejipanga kutoa huduma hiyo kwa ufanisi mkubwa ambapo pamoja na vipimo vitakavyofanyika pamoja na ushauri wa afya ya macho watafanya opareshini ya macho siku hiyo hiyo kwa wale wote watakaogundilika na tatizo hilo.
" Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 50 Kuna shida ya mtoto wa jicho kwa upande wa Tanga ndio maana tumeita wadau wetu ili waje kusaidia wananchi na tutakuwa na madaktari bingwa kutoka sehemu mbalimbali, kama kuna mtu anahitaji upasuaji AA macho atafanyiwa siku hiyo hiyo bila malipo" alisema Dkt Hussein.
Post A Comment: