Na Hadija Bagasha Korogwe,
Baadhi ya wananchi wanaoishi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wamesema wanaokabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo za Ardhi, Mirathi, na masuala ya ukatili wa kijinsia ambazo zimeshindwa kupatiwa ufumbuzi kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kutumia vizuri madaraka yao.
Kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid wameweza kupatiwa elimu na hatimaye kupatiwa majawabu ya changamoto zao.
Timu ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imefika katika Kanisa Katoliki jimbo la Tanga Parokia ya mtakatifu Augustino Manundu lililopo katika Halmashauri ya Korogwe Mji Mkoani Tanga na kutoa elimu kuhusu, Ukatili wa kijinsia, Haki za watoto, Utatuzi wa migogoro ardhi na ya kifamilia.
Akizungumza na kituo hiki mmoja wa wananchi hao Leogard John mara baada ya kupatiwa elimu hiyo baadhi ya wananchi hao wamesema wanamshukur Rais Dkt Samia kwa kusikiliza shida za wananchi na kutoa timu hiyo ambayo imekuwa na matokea chanya kwa wananchi wanyonge ambao walikuwa wanakosa sehemu ya kufikisha changamoto zao.
"Nchi ya Tanzania ni kubwa watu wengi wanachangamoto mbalimbali wanashindwa kujua waende wapi ili kueleza shida na kero zao wakati mwingine kuna wengine wananyanyasika kutokana na baadhi ya viongozi kutumia vibaya madaraka yao hata wakienda hawasikilizwi, "alisisitiza Mwananchi huyo.
"Kwa nafasi hii Rais wetu mpendwa umetuletea hawa watu kwenye maeneo yetu wamekuja kutusikiliza na kutupa elimu juu ya matatizo yetu wametuhudjmia vizuri hususani sisi wananchi wanyonge tuliosumbuka kwa kipindi kirefu bila kujua wapi pa kwenda kuelezea shida zetu, "alibainisha John.
Kwa upande wake Kiongozi wa timu ya utekelezaji wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia Katika Halmashauri ya Korogwe Mji Wakili George Banoba amesema kwamba dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona kwamba Tanzania bila migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa na bila ukatili inawezekana.
"Mheshimiwa Rais ametutuma sana ili tuweze kuwaelimisha wananchi watambue haki zao na namna ya kuzipata kama wamedhulumiwa au kupokonywa kujua wanaweza kuzipata kwenye taasisi zipi na ndio maana kampeni hii inaongozwa na kauli mbiu isemayo msaada wa kisheria kwa haki, usawa, Amani na maendeleo, "alisema Wakili Banoba.
"Kwa kifupi wananchi wamemshukudu sana, Rais Dkt Samia kwa kuwaletea kampeni hii ambayo imekuja wakati muafaka, "alisisitiza.
Mwisho.
Post A Comment: