Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Arusha Mhe. Ojung'u Piniel Salekwa leo tarehe 23/04/2025 imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe. Ojung'u Salekwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kushauri timu ya wataalamu kwa kushirikiana na wasimamizi wa miradi kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ukarabati wa Madarasa ya Shule ya Msingi Laroi ambapo jumla ya majengo 08 yatakarabatiwa, ujenzi wa Matundu 12 ya vyoo vya Wanafunzi na vyoo vya Waalimu ambapo mpaka kukamilika kwakwe utagharimu kiasi cha shilingi 76,000,000/=.
Pia kamati hiyo ilitembelea ujenzi wa Chumba cha Kuhifadhi Maiti katika Kituo cha Afya Oljoro ambapo ujenzi huo upo hatua ya umaliziaji na unagharimu kiasi cha Shilingi 40,000,000 ikiwa ni fedha kutoka Mapato ya Ndani.
Aidha Kamati hiyo ya fedha ilitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa matundu 24 ya vyoo katika shule ya Msingi Mirongoine ambapo ujenzi huo upo katika hatua ya umaliziaji ambapo kiasi cha shilingi 55,923,458 fedha kutoka Serikali Kuu.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Matevez ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Mhe.Freddy Ezekiel amewataka Wataalam wa Halmashauri idara ya Uhandisi kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa Miradi hiyo ili iweze kukamilika na kuwa na manufaa kwa wananchi.
Akizungumzia miradi hiyo,Diwani wa Kata ya Olturoto mhe.Baraka Simeon amewapongeza Wataalam kwa kazi nzurii wanayofanya ya kusimamia Miradi hiyo na kuwataka kuzingatia ubora wa majengo na kuitaka kamati za Ujenzi kuwa kuelejeza nguvu zao katika usimamizi.
Naye Diwani wa Kata ya Olturumet Mh Joseph Tinayo amewataka wananchi ambao miradi hiyo inatelekezwa kwenye maeneo yao kutoa ushirikiano wakutosha kwa Wataalam,mafundi kwani mara baada ya kukamilika itakuwa chini ya uangalizi wao katika kuitunza.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Daktari Petro Mboya ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo ameishukuru Kamati ya Mipango Fedha na Uchumi kwa kutembelea Miradi hiyo na kuhaidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliotolewa na Kamati na kuahidi kufanyia kazi haraka.
Post A Comment: