Mkurugenzi wa Kampuni ya R-GI CO LTD ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya vito FEMATA Ndg. Prosper Tesha, Ameishukuru serikali kwa kuwapatia umeme migodini kitu ambacho kimeleta mabadiliko makubwa na ya uhakika katika sekta ya madini.

Aidha ameeleza kuwa katika awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya madini imeweza kuchangia pato la Taifa kwa 10.1% hadi kufika mwaka wa fedha 2024 /2025 kitu ambacho kimetokana na sera, na usimamizi mzuri wa Wizara ya madini chini ya Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde na wasaidizi wake.

Aidha mwenyekiti huyo ameeleza kuwa hadi sasa wachimbaji wote wa madini ya vito nchini ni zaidi ya milioni sita na watanzania wengi bado wanahamasika kuingia katika sekta ya madini kuendelea kunufaika na rasilimali za Taifa la Tanzania.

"Tumekubalia na Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wa madini nchini Ndg. Johm Wambura Bina na wanachimbaji wote tulidhia kuunga mkono serikali ya awamu ya sita kubaki madarakani na kupiga kura za ndiyo za kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kishondo kwa kura zote ambazo ni zaidi ya milioni sita.


Aidha ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan wamejivunia na kuona mabadiliko makubwa katika Sekta ya Madini pamoja na sekta nyingine zinazo husu jamii na kufanya taifa kuwa lenye mafanikio makubwa kiuchumi.

Aidha kwa upande wake Mwekezaji na mchimbaji wa madini hayo adhimu ya ruby Ndg. Sendeu Laizer amekabidhi madawati 300 katika shule za kata ya mundarara ambapo ameeleza kuwa huo ni muendelezo wa kurudisha kwa jamii kutokana na faida alizopata katika uchimbaji huo wa madini ameweza kurudisha kwa wananchi zaidi ya milioni 500.


"Naishukuru serikali baada ya kupata madini na kutangazwa kuwa bilionea, Serikali iliweza kunishauri namna bora ya kuendeleza mtaji huu na mafanikio nimeyaona hadi leo kampuni yangu tunaendelea kuchangia kwa jamii na leo hii naikabidhi serikali madawati 300". Amesema Sendeu.




Share To:

Post A Comment:

Back To Top