NA: STELLA NGENJE-NAMTUMBO

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM na Mgombea Mwenza wa Urais 2025 Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi,amewashukuru wananchi wa Namtumbo kwa mapokezi ya Kishindo,akipeleka pia salamu za upendo za Mwenyekiti wa Chama Taifa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani,ametumia nafasi hiyo pia kueleza namna ambavyo anafurahishwa Mno na uhai wa Chama cha Mapinduzi,ambacho kinaendelea kujibu changamoto za Wananchi.

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo April 03,2025 Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma Wakati akizungumza na Wananchi,amewapongeza Wananchi wa Namtumbo kwa kushika nafasi ya  pili Kimkoa katika Mkoa wa Ruvuma kwa uzalishaji wa Mazao ya aina mbalimbali,wakishika pia nafasi ya kwanza kwa uzalishaji wa zao la Tumbaku”Mnatoa heshima kubwa kwa Mkoa wenu kwa uchapakazi wenu kwa uchapakazi wenu,endeleeni kuchapakazi tunajivunia,tukisema tunatoka Mkoa wa Ruvuma halafu tunaanza kutaja Wilaya zetu kwa Mbwembwe kwa sababu tunajua Mnalinda heshima ya Nchi yetu,tuendelee kuchapakazi tukijua kazi ni kipimo cha utu”


Katibu Mkuu wa CCM amesema Miaka 10 Mfululizo Tanzania inajitosheleza kwa Chakula,akiutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa ni miongoni mwa Mikoa Mitano (Big 5) hapa Nchini ambayo inazalisha chakula kwa Wingi,hivyo amewakumbusha Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) na Wizara ya Kilimo Nchini Kuhakikisha Wakulima wanapata Mbegu kwa urahisi kwa kuzisambaza kwa wakala walio karibu yao.amewataka ASA Kuongeza uzalishaji wa Mbegu hizo.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vitta Kawawa ametumia nafasi hiyo Kuishukuru Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kwa kujibu Changamoto za Maji Namtumbo ambapo ametoa zaidi ya Bilioni 7 na Utekelezaji wa Mradi huo utaanza muda mfupi ujao,ameshukuru kwa miradi mingine iliyotekelezwa Jimboni kwake ikiwemo miradi ya Shule za Sekondari zimejengwa na Madarasa 207,zaidi ya Bilioni 6 zikitumika kwenye Sekta ya afya,akiutaja pia upungufu wa Watumishi nakuwepo kwa baadhi ya changamoto za Barabara ya Mtwara pachani kwenda Lusewa Mpaka Tunduru akiomba itengenezwe kwa Kiwango Cha Lami,Barabara ya pili ni lumecha,Hanga ,Kitanda kwenda Mpaka Malinyi kutokea Ifakara.


Mhe.Vitta Kawawa amemuomba Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi Kufikisha ombi lake kwa Serikali ya Dkt. Samia,akiomba  kupigwa jeki ya ujenzi wa Soko pamoja na Stend ya Mabasi Namtumbo”Mhe. Katibu Mkuu sisi pia hapa Namtumbo tuna shida ya Soko sisi hapa Mjini hatuna Soko wala Stend ya Mabasi,tunaomba sana hili Katibu Mkuu utusimamie Serikali tupate fedha tuweze  tujenga Soko hapa,Watu wanahangaika kuuza mazao yao,sisi ni wakulima na tuna mazao mengi,tunaomba sana Katibu Mkuu uweze kulifanyia kazi”


Akijibu maombi hayo,DkT. Nchimbi ameielekeza Serikali ianze mchakato wakufuatilia jambo hilo nakuanza kujua Wananchi wa Namtumbo nao wana haki yakupata Soko la Kisasa au Stend ya Kisasa,”ni vizuri eneo kubwa hili kuwa na Soko pamoja na Stend,Serikali itaangalia kipaumbele lakini vitu hivi ni muhimu vifanyike,na nitakuwa nikiwaunga mkono Wananchi wa Namtumbo kuhakikisha kwamba tunafuatilia mahitaji yenu haya yanafanyika,lakini pia Changamoto alizozisema za Barabara nimezisikia nitaendelea kuzifanyia msukumo wa kipekee nakuzifanyia kazi”

Aidha Dkt.Nchimbi amebainisha kwamba CCM inalo Jukumu lakuendelea kuandaa Vijana ambao ndio Viongozi wa Kesho,akisisitiza kwamba  Uhai wa Chama ndio injini ya ushindi Miaka na Mikaka,na nilazima kuona Chama kinatimiza wajibu wake kwa Wananchi,kujali kero na matatizo ya wanyonge wa kawaida,ametilia mkazo kuhakikisha CCM Inaendelea kuandaa vijana, ambao watashika nyazifa mbalimbali za uongozi ili Chama cha Mapinduzi kiendelee kushika dola nakuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea Maendeleo.

Dkt. Nchimbi yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya Kikazi ya siku 5 akitokea Mkoani Mtwara, Jana April 02 alikuwa Wilayani Tunduru,Leo April 03 alikuwa Namtumbo,ziara hii atahitimisha Aprll 6 kwa kutembelea baadhi ya vitega uchumi vya Chama vilivyopo Songea Mjini,na kisha atazungumza na Wananchi akiwa kwenye kata ya Mshangano.

Share To:

Post A Comment: