Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bi. Rose Robert Manumba amefanya ziara ya kutembelea vyanzo mbalimbali vya mapato yatokanayo na  wachimbaji wa madini ya dhahabu  10\/4\/2025, katika ziara hiyo Mkurugenzi Manumba aliambatana na Wataalamu mbalimbali kutoka ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Msalala.

Aidha katika ziara hiyo Mkurugenzi Manumba amesikiliza changamoto mbalimbali walizo nazo wadau na wamiliki wa shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu pamoja na kuzitatua  changamoto hizo

Pia Manumba amewasisitiza wadau hao juu ya umuhimu wa ulipaji wa ada, tozo na Ushuru  mbalimbali ili kufanikisha shughuli  mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali.

Nae Afisa Mapato wa Halmashauri ya Msalala Bw. Msosole Salehe ametoa elimu juu ya namna sahihi ya ulipaji na ushiriki wa wadau hao katika shughuli mbalimbali za kijamii na kuwasisitiza kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jamii inayo wazunguka na Halmashauri nzima.








Share To:

Post A Comment: