Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM bara, Ndugu Mussa P. Mwakitinya, amesema kuwa uongozi wa sasa wa CHADEMA ni wa kiharakati zaidi kuliko kutatua changamoto za Watanzania.Uongozi wa zamani ulitumia meza ya majadiliano kujenga, lakini sasa kuna mwelekeo wa kubomoa badala ya kujenga.
Kwa upande mwingine, Ndugu Mwakitinya amesisitiza kuwa kwenye meza ya majadiliano hakuna kinachoshindikana.
Amewaasa wanasiasa kutoka vyama vyote kutumia busara zaidi katika kutatua changamoto za Watanzania, kwani CCM inajivunia kutatua matatizo ya wananchi na inakaribisha mawazo ya kujenga ili kuleta mabadiliko chanya.
Pia, alikumbusha kuwa majadiliano hayakufanyika bure, kwani yalileta matunda muhimu kwa nchi. Majadiliano yameongeza uhuru wa vyombo vya habari, ambayo ni nguzo muhimu katika demokrasia.
Aidha, majadiliano hayo yameongeza ufanisi wa utawala bora na umoja na ndiyo yaliyopelekea kuundwa kwa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Mwaka 2024, ambayo ni hatua muhimu katika kuhakikisha uchaguzi huru na haki kwa Watanzania, Majadaliano yamepekea kuwepo kwa mikutano ya hadhara na Maandamano ya kisiasa
Post A Comment: