Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo na Uvuvi Mhe. Deodatus Mwanyika kwaniaba ya Bunge la Tanzania ameeleza kuwa Chombo hicho cha kusimamia na kuishauri serikali, kimeridhika na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zilizotekelezwa kwenye miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wakati akitoa salamu za Bunge kwenye hafla ya uzinduzi wa Benki ya Taifa ya Ushirika leo Jumatatu Aprili 28, 2025,Mhe. Mwanyika kwaniaba ya Spika wa Bunge Tulia Ackson, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pia kwa utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayoibuliwa na wabunge ikiwemo ambayo yalikuwa yakionekana kuwa magumu katika kutekelezwa kwake.
" Moja ya mambo tuliyoyasema muda mrefu Bungeni na mengine yamesemwa kwa miaka mingi bila kutekelezwa lakini serikali yako imetekeleza ni suala la bajeti ya Kilimo kuongezwa, serikali yako imeongeza bajeti hiyo kutoka Bilioni 290 hadi Shilingi Trilioni 1.24, jambo hili ni kubwa na limewezesha mambo mengi mengine kufanyika. Itoshe kusema Bunge tunatambua mchango wako mkubwa." Amesema Mhe. Mwanyika.
Katika hatua nyingine pia Mwanyika amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia kwa usikivu wake na kuchukua hatua za haraka kwenye masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi na yanayoibuliwa na wabunge, akimpongeza pia kwa kutekeleza sehemu ya malengo na mipango yake mingi aliyoieleza Bunge Aprili 2021 wakati alipohutubia kwa mara ya kwanza mara baada ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akichukua Uongozi kwa mtangulizi wake hayati Dkt. John Magufuli.
Post A Comment: