Bunge limeipongeza Serikali na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, kwa kuchukua hatua za haraka kurejesha mawasiliano kwenye barabara ya Kusini.
Akizungumza bungeni leo, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, amesema hatua zilizochukuliwa za kurejesha mawasiliano zimepunguza mateso kwa wananchi na kuruhusu kuendelea kwa shughuli za uchumi.
Tangu kuharibiwa kwa barabara hiyo kutokana na mvua zillizosababisha mafuriko, Ulega na watendaji kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) waliweka kambi katika maeneo ya Somanga Mtama na Matandu ili kurejesha usafiri katika hali ya kawaida.
Naibu Spika pia amewapongeza mawaziri wote walioshiriki katika kuhakikisha mawasiliano yanarejea kwa wakati.
Post A Comment: