NAIBU Waziri Mkuu wa Waziri wa Nishati, Dk, Dotto Biteko amesema viongozi mbalimbali watakaobainika kuuza ardhi au kuleta migogoro kwa wananchi watachukuliwa hatua pale itakapobainika.

Aidha amesema serikali itafanya kila namna kuhakikisha wafugaji nchini wakiwemo wa wilaya ya Monduli wanaendelea kuimarika na kuheshimika na kuwa daraja la juu kwa sababu mifugo yao inatathamani na inachangia pato la taifa kwa asilimia saba.

Dk, Biteko aliyasema hayo Wilayani Monduli katika ziara yake wilaya za Arusha kuelekea maadhimisho ya sherehe za miaka 61 ya Muungano wakati akiongea na wananchi shule ya sekondari Migungani One iliyopo wilayani hapo. 

Alisisitiza viongozi wa serikali kazi yao kubwa ni kuhudumia wananchi kwa haki na kuepuka kuuza ardhi za watu na mahali popote na itakapobainika kiongozi kauza ardhi basi sheria ichukue mkondo wake na kusisitiza viongozi kuacha kulumbana badala yake wafanye kazi kwani wananchi wanahitaji maendeleo na si malumbano. 

"Kiongozi atakayebainika kuuza ardhi ya wananchi au kuleta migogoro ya ardhi atachukuliwa hatua na naipongeza wilaya ya Monduli kwa kutatua kero za ardhi na wilaya hii itakuwa ya mfano katika utatuzi wa migogoro ya ardhi"

Alisema katika kuhakikisha wananchi haswa wafugaji mifugo yao inakuwa yenye tija zaidi na kupata maeneo ya malisho na maji serikali imekuwa ikiweka malambo na majosho kwaajili ya mifugo hiyo kupata maji

Alisema serikali inatambua umuhimu wa wafugaji na kuhakikisha wafugaji hao wanakuwa na maendeleo ikiwemo uchumi kukua zaidi

"Mimi ni mfugaji,nimesoma na kulelewa kwa kuuza maziwa na hiyo hii ndiyo biashara ninayoifahamu na Rais Dk,Samia anawapenda wafugaji na ndiyo sababu anahakikisha penye miradi ya maji pia mifugo inapata maji ya kunywa"

Kuhusu umeme alisisitiza serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha umeme huo unawafikia wananchi Ikiwemo wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kwa kujenga kituo cha kusambaza umeme njia tank pamoja na kituo cha kupoozea ili kuhakikisha nishati hiyo inawafikia pasipo kukatikatika. 

"Najua kuna uchaguzi Mkuu unakaribia watu watapitapita hapa kusema maneno yao wasikilizeni kisha angalieni nani anafaa tuungane tujenge taifa letu ikiwemo amani nashangaa baadhi ya viongozi kutumia muda mrefu kugombana badala ya kuhudumia wananchi "

Wakati huo huo akiwa shule ya sekondari Migungani one alisema elimu ni msingi mkubwa wa maendeleo kwani serikali inathamini elimu hivyo wazazi na walezi wanajibu mkubwa wa kuwapatia elimu watoto elimu kwani ndio msingi wa maendeleo

Alisema watoto zaidi ya 8,200 wanasoma hapo kwani shule hiyo ya sekondari Migungani one itakuwa na uwezo wa kuwa na idadi ya wanafuzi 4000 na kuwasihi wanafunzi hao kuwa na nidhamu ikiwemo kusikiliza walimu hao

"Nimefurahi kusikia wanafunzi 82 wa kike ambao awali walikuwa wamepangwa shule za mbali wamehamishiwa hapa hivyo ni vyema shule hii ikawekwa uzio ili wanafunzi wa we salama zaidi kutokana na wanyama wakali".

Alipongeza wilaya hiyo kwa utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa kuwa na kitengo cha kusikiliza kero na kusisitiza wilaya hiyo kuwa shamba darasa kati ya wilaya nyingine huku akisisitiza serikali itatenga fedha kwaaajili ya kujenga uzio katika shule ya sekondari Migungani one ili kuzuia wanyama wakali wasilete madhara kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo

Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga alisema wilaya hiyo inakabiliwan a changamoto ya migogoro mikubwa ya ardhi kutokana na ufugaji lakini kadri siku zinavyozidi kwenda wanaitatua migogoro hiyo ili kuhakikisha wafugaji wananufaika kwani wenye fedha ndio wananunua ardhi wilayani hapo na kuleta mkanganyiko kwa wananchi hao.

"Migogoro mikubwa ni ardhi lakini kadri siku zinavyoenda tunaitatua lakini pia tunaishukuru serikali kwa kuhakikisha umeme unapatikana pamoja na fursa za uwekezaji kupitia utalii"

Aliishukuru serikali kwa kuhakikisha miradi mbalimbali inakamilika sanjari na upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi hao huku akisisitiza mradi wa magadi soda eneo la Engaruka kuwa na manufaa zaidi kwa nchi na wananchi wa wilaya ya Monduli na Mkoa wa Arusha

Alitoa onyo kali kwa mashirika yasiyo ya serikali (NGOs)yanayopotosha mradi huo wa magadi soda eneo la Engaruka na kusema kuwa serikali haitasita kufungia mashirika hayo hizo zinazopotosha mradi huo

"Arusha ni moto na wananchi wake ni wa moto pia na mwaka huu wa uchaguzi ni mwaka ambao ilani imetekelezwa na wananchi wameona hivyo tunaomba mpelekee salamu Rais Samia Hassan Suluhu kuwa wananchi wameona kazi anazofanya na watamlipa kwa kura nyingi"

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Hapiness Laizer aliishukuru serikali kwa ujenzi wa miundombinu ya shule Moya ya sekondari Migungani One ambayo ni jengo la uta wala, madarasa name, jengo la maktaba, jengo la Tehama, maabara tatu , vyoo na matundu kumi 












Share To:

Post A Comment: