Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma amezindua rasmi Baraza jipya la Uongozi wa IAA leo tarehe 7 April 2025 

Akizungumza katika hafla hiyo Mheshimiwa Waziri Dkt. Riziki amelipongeza Baraza hilo kwa kuchaguliwa kuiongoza IAA na kuwasisitiza kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia maadili ili kukiletea maendeleo Chuo na jamii kwa ujumla

“Wenye taaluma kama mlizonazo Tanzania ni wengi ila ninyi mmeaminiwa hivyo hakikisheni mnatekeleza majukumu kwa kuzingatia misingi ya uwazi, na ushirikiano ili kuleta mabadiliko makubwa Zaidi ndani ya Chuo” amesema Dkt. Riziki

Pia Dkt. Riziki ameupongeeza Uongozi wa Chuo kwa jitihada wanazozifanya kuendelea kuboresha mitaala, pamoja na miundombinu huku akivutiwa na nafasi za uongozi wanazopewa wanawake na kusisitiza waendelee kuaminiwa kwani wana nguvu kubwa katika kukuza uchumi hapa nchini

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi IAA Dkt. Mwamini Tuli amewakaribisha wajumbe wapya katika bodi hiyo na kuwaomba ushirikiano hasa katika ufanyaji kazi kwa kuzingatia maadili, ubunifu na kujitoa ili kuhakikisha Chuo kinapata maendeleo Zaidi

“Jukumu letu ni kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya kujifunza na kujifunzia, kuendeleza miradi mingine ya Chuo lakini kuhakikisha IAA inafika mbali kitaifa na kimataifa hivyo tushirikiane kutekeleza majukumu haya” amesema Dkt. Mwamini

Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka amesema IAA inatambua kazi kubwa inayofanywa na Bodi na ndio chanzo cha hapa walipo kwa sasa hivyo wanaahidi kuwapa ushirikiano kwa asilimia mia moja ili kufikia malengo waliyojiwekea

Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa baadhi ya mambo makubwa yaliyofanyika kwa miaka mitatu iliyopita ni pamoja na idadi ya mwanafunzi kuongezeka kutoka 13000 hadi 19000, Mitaala 115 mpaka 140 lakini pia miundombinu ya majengo katika kampasi mbalimbali za Chuo inayoendelea kujengwa












Share To:

Post A Comment: