Moja ya Majengo ya zamani katika Shule ya Wasichana ya Ashira iliyopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ,miongoni mwa shule Kongwe zilizofanyiwa maboresho ya miundombinu ya Madarasa,Mabweni pamoja na Vyoo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira Zainabu Shushue akizungumzia maboresho yaliyofanywa na Serikali kupitia Mbunge wa Jimbo la Vunjo Dkt Charlwes Kimei katika shule hiyo
kongwe .


Dada Mkuu katika Shule ya Wasichana ya Ashira ,Prisca Baraka (Mwenye miwani) akizungumzia maboiresho yaliyofanyika shuleni hapo .
Muonekano wa baadhi ya Majengo ya Madarasa na Mabweni yaliyojengwa katika Shule ya Wasichana ya Ashira iliyopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimannjaro
Na huu ndio muonekano wa sasa wa Vyoo vilivyojengwa katika shule ya Wasichana ya Ashira iliyopo Marangu wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro .
Bwalo ambalo kwa sasa ujenzi wake unaendelea katika shule hiyo .




Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ashira, moja ya shule kongwe katika Mkoa wa Kilimanjaro, sasa wanapumua kwa afueni baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa miundombinu mipya ikiwemo mabweni, madarasa na vyoo.

Kwa miaka mingi, shule hiyo ilikuwa ikikumbwa na changamoto ya msongamano katika mabweni na madarasa, hali iliyokuwa ikiathiri moja kwa moja mazingira ya ujifunzaji.

Lakini hali hiyo imeanza kubadilika kwa kasi baada ya serikali kutoa zaidi ya shilingi milioni 269.7 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha miundombinu shuleni hapo inayoendelea kuboreshwa ndani ya kipindi cha miaka minne.

Akizungumza na Wnahabari , Dada Mkuu wa shule hiyo, Prisca Saimon Baraka, alisema kuwa ujio wa madarasa na mabweni mapya umeleta mabadiliko chanya katika maisha ya kila siku ya wanafunzi.

"Wakati najiunga na Ashira, tulikuwa tunabanana sana mabwenini na kwenye madarasa. Lakini sasa kila darasa lina wanafunzi wachache na mazingira ni rafiki kwa kujifunza. Hii imerahisisha kazi kwa walimu na imetuongezea morali ya kusoma," alisema Prisca.

Naye Belinda Ndosi, mwanafunzi wa kidato cha sita, aliongeza kuwa hali ya awali ya msongamano kwenye vyoo ilikuwa ya kusikitisha.

"Kabla ya ujenzi huu, kulikuwa na foleni ndefu chooni. Lakini sasa kila mtu anaweza kutumia choo kwa wakati na kwa heshima. Tunaishukuru serikali, na zaidi Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali elimu ya mtoto wa kike," alisema Belinda.

Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Zainabu Shushue, fedha zilizopokelewa zilitumika kujenga madarasa matano, choo chenye matundu saba na bweni moja.

Miundombinu hiyo tayari imeanza kutumika na imeleta tija kubwa katika kuboresha taaluma ya wanafunzi.

"Shule yetu ina jumla ya wanafunzi 820. Kupitia mradi huu, tumeweza kupunguza msongamano na kurahisisha kazi ya ualimu, hasa kwa wale wanafunzi wanaohitaji msaada wa ziada darasani," alisema Bi. Shushue.

Aliongeza kuwa shule inatarajia ongezeko la wanafunzi hadi kufikia 900 mwaka 2025, hivyo ipo haja kwa serikali kuongeza mabweni zaidi ili kukidhi mahitaji ya makazi ya wanafunzi wapya.

Wanafunzi wanasema miundombinu hiyo ni chachu ya mafanikio na inaendana na dhamira ya taifa ya kumwezesha mtoto wa kike kupata elimu bora katika mazingira salama.

Ashira Girls Sekondari imekuwa ni miongoni mwa shule zinazofaidika na juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia nchini kupitia miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu
Share To:

Post A Comment: