Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka minne ya Uongozi wake imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 956 kwaajili ya utekelezaji wa miradi takribani 1360 ya maendeleo katika maeneo mbalimbali Mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Nurdin Babu ametoa kauli hiyo leo Machi 09, 2025 wakati wa hotuba yake wakati wa Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe, ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye anayeweka jiwe la msingi wa mradi huo mkubwa uliogharimu takribani Bilioni 300.

Katika maelezo yake, Mhe. Nurdin Babu ameahidi ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu ujao mwezi Oktoba 2025 kutokana na utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo, akisema ushindi wake utafanana na ule uliovunwa na Chama Cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Wakati CCM iliposhinda viti vyote vya Wenyeviti wa serikali na mitaa kwenye Vijiji vya wilaya za Same na Mwanga.

Mhe. Mkuu wa mkoa pia amewahimiza wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika michakato yote ya uchaguzi huo na Kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kutetea nafasi yake, akiahidi usalama na utulivu wa kutosha kwa kila mwananchi wakati wa Uchaguzi huo.

Share To:

Post A Comment: