Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameuelezea mchango mkubwa wa aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Wizara ya Madini Marehemu Edson Nkongo katika kuboresha na kuongeza Makusanyo ya Maduhuli ya Sekta ya Madini.

"Edson kwa kushirikiana na wenzake, alianzisha mifumo bora ukiwemo wa Masoko ya Madini, ambao umeleta mageuzi makubwa katika ukusanyaji wa maduhuli na kueleza kuwa umesaidia kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli kutoka shilingi bilioni 116 hadi kufikia shilingi bilioni 753 katika Mwaka wa Fedha 2023\/24 ,  na kuongeza mwaka huu tunatarajia kukusanya shilingi trilioni moja," amesema Waziri Mavunde.

Ameyasema hayo leo Machi 15, 2025 wakati akitoa Salam za rambirambi  za Wizara  kumuaga mtumishi huyo aliyefariki dunia Machi 12, 2025 katika  Hospital ya Tumbi- Kibaha  alipokuwa akipatiwa matibabu na kusema, Edson anabaki kuwa nguzo  kuu kwenye mabadiliko  ya Sekta ya  Madini na kwamba utaalam wake  umeisaidia nchi.

‘’Edson alikuwa mbunifu aliyejua anachopaswa kufanya, atabaki kwenye kumbukumbu zetu. Kupitia yeye na wenzake, amesaidia kuongeza mapato ya sekta kutokana na mifumo aliyoianzisha, hali ambayo ilifanya nchi nyingi kuja nchini kujifunza,’’ amesema Waziri Mavunde.

Ameongeza kwamba mbali ya mifumo inayotumiwa katika Sekta ya Madini, pia alihusika katika kamati za kitaifa kuandaa mifumo mingine ikiwemo mfumo wa Luku wa Tanesco na kuongeza, Serikali na Wizara tumepata pigo,’’ amesema Waziri Mavunde.

Akisoma wasifu wa marehemu Edson kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini Augustine Olal amesema  marehem Edson  alifanya shughuli za mfano ikiwemo kuanzisha mfumo wa Local Content kwa kushirikiana na wenzake na kumweleza kuwa alikuwa mtumishi mwenye bidii ya kazi na mwadilifu.

Share To:

Post A Comment: