Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana,ajira na watu wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete leo machi 11 amefanya ziara ya kutembelea na kugagua eneo la uwanja wa shirika la elimu Kibaha ambao utatumiaka katika sherehe za uwashwaji wa Mwenge wa uhuru Kitaifa ambapo baada ya kupita ameridhishwa sana na maandalizi ambayo yanaendelea kufanyika katika uwanja huo.


Ridhiwani ameyasema hayo wakati alipofanya ziara kwa ajili ya kutembelea na kugagua mwenendo na maandalizi katika eneo la uwanja wa shirika la elimu Kibaha ambapo utatumika kwa ajili ya uwashwaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ikiwa sambamba na kuzungumza na vijana hao na kuwahimiza kuwa wavumilivu katika kipindi chote cha maandalizi.

"Nimeridhishwa sana na maandalizi yanayofanyika katika eneo hili la uwanja wa shirika la elimu Kibaha ambapo kutafanyika tukio kubwa la sherhe za uwashwaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa na kwamba nimeweza kuona mwenendo mzima wa ukarabati wa uwanja huo ikiwa pamoja na kupata fursa ya kuzungumza vijana wa halaiki,"amesema Ridhiwani Kikwete.

Kadhalika Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wa halaiki ambao wamechaguliwa kushiriki katika maandalizi ya uwashwaji wa Mwenge wa uhuru Kitaifa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuwa wazalendo na nchi yao na kutunza na kuzilinda rasilimali za Taifa.

Naye Injinia kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Charles Kabeho ambaye pia ni msimamizi wa ukarabati wa eneo la uwanja utakaotumika kuwashiwa Mwenge wa uhuru amebainisha kwamba kwa sasa ukarabati kwa sasa umeshafikia asilimia 75.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amebainisha kwamba maandalizi yote kwa ajili ya kuelekea katika tukio la kuwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa yanaendelea vizuri katika maeneo ya miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, maji na kwamba hadi sasa hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa kwa kiwango kikubwa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kwamba wamejipanga vizuri na kwamba wanatarajiwa kukabidhiwa rasmi uwanja huo amabo utatumika kwa ajili ya sherehe za uwashwaji wa Mwenge wa uhuru Kitaifa na kuwahimiza wananchi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi siku hiyo.


Sherehe za uwashwaji rasmi wa Mwenge wa uhuru kitaifa zinatarajiwa kufanyika rasmi Aprili 2 mwaka huu katika viwanja vya shirika la Elimu Kibaha vilivyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ambapo viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki katika tukio hilo.



Share To:

Post A Comment: