Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amepongeza ubunifu wa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) chini ya kiatamizi cha IAA Business Startup (IBSUC) akiahidi kutembelea chuo ili kuona kwa karibu jinsi kinavyowalea wajasiriamali vijana na kuwaandaa kukabiliana na changamoto za ajira na maendeleo ya jamii
Maonesho haya ni sehemu ya maandalizi ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kitaifa yataadhimishwa tarehe 8 Machi 2025, jijini Arusha, hafla inayotarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kama mgeni rasmi
Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe haki, usawa na uwezeshaji", ikilenga kuwainua wanawake na wasichana katika nyanja za elimu, uchumi na teknolojia.
Post A Comment: