Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameshiriki uzinduzi wa ujenzi wa visima vya maji nchini ili kusaidia kuwezesha kilimo cha umwagiliaji .
Uzinduzi huo ulioongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi .Rosemary Senyamule umefanyika hii leo katika kata ya matumbulu Mkoani hapa ikiwa ni mojawapo ya maeneo yaliyopo ndani ya mradi ambapo visima 68,000 vinatarajiwa kuchimbwa nchi nzima.
Aidha Mavunde ametoa pongezi kwa Waziri wa kilimo na Tume ya umwagiliaji kwa jitihada walizozionesha katika kuwasaidia wakulima wa zabibu mkoani hapa kuondokana na kazia ya ukosefu wa maji katika mashamba yao .
"Yote haya yanafanyika hapa lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima wa zabibu anapata soko la uhakika ,natamani kumuona mkulima wa zabibu kawa na maringo na zabibu yake "alisema Waziri Mavunde .
Post A Comment: