Na Imma Msumba : Arusha 

NAIBU Waziri Mkuu,Dotto Biteko amesema kuwa wananchi wa Tanzania wanataka kujua rasilimali zao za nchini zinawanufaishaje hivyo ni wajibu wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibukaji katika rasilimali za Madini na Gesi Asili{EITI} kuhakikisha kuwa kampuni zote zilizowekeza katika sekta hizo hapa nchini kuweka wazi mapato yake ikiwa ni njia mojawapo nya uwajibikaji.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani,Innocent Mashingwa kwa niaba ya Biteko wakati akifungua Kikao cha 62 cha Bodi ya EITI Duniani kilichofanyika Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na nchi wanachama 52 Duniani.

Biteko alisema nchi ya Tanzania ina rasilimali nyingi katika sekta ya madini na Gesi asilia na kampuni nyingi zimewekeza katika sekta hiyo hivyo ni wajibu wa kampuni hizo kueleza kwa uwazi mapato yanayopatikana katika shughuli zao za kila siku.

Alisema Tanzania imejiunga na EITI mwaka 2009 na ilikuja kubadili sheria mwaka 2015 ya kutaka kila kampuni inayowekeza katika sekta hizo kuweka wazi mapato wanayopata ili wananchi waweze kujua kwa kiasi gani rasilimali za nchi zinawanufaisha.

Naibu Waziri alisisitiza na kuwataka wawekezaji kuwekeza katika sekta za madini na Gesi Asilia kwa kuwa sera zake ni za uwazi na zenye manufaa na pia aliwataka wawekezaji kujikita katika sekta ya Utalii kwani sekta hiyo kwa sasa inajulikana kote nchini kufuatia filamu ya The Royal Tour ilizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kutangazwa kote Duniani na kuvutia watalii wengi hapa nchini.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan amejenga mazingira mazuri na rafiki kwa kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya madini,Nishati na Gesi Asilia hivyo EITI inapaswa kusisitiza wawekezaji kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji katika ukusanyaji mapato.

Naye Waziri wa Madini,Antony Mavunde alisema kuwa hatua ya Rais kuimarisha Diplomasia katika kipindi chake cha muda mfupi kumefanya mikutano mingi ya Kimataifa kufanyika nchini hatua ambayo serikali inanufaika na mikutano hiyo.

Mavunde alisema eneo la uwazi na uwajibikaji ni eneo nyeti kwa rasilimali za nchi hivyo ni wajibu wa wawekazaji kuweka wazi mapato yao ili wananchi wawezee kujua wananufaika vipi na rasilimali zao za nchi.

Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu {CAG}mstaafu,Ludovick Utouh ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya EITI alisema kufanyika kwa Kikao hicho nchini ni faida kubwa kwa nchi kwani haijawahi kutokea toka Tanzania ilipojiunga na Bodi hiyo mwaka 2009.

Alisema Bodi ya EITI hadi sasa imetoa ripoti 14 mbalimbali hadi sasa katika utendaji kazi wao na june mwaka huu inatarajia kutoa ripoti ya 15 hivyo wanajivunia kwa utendaji wao wa kila siku na wanasisitiza uwazi na uwajibikaji kwa wawekezaji katika kila nchi.








Share To:

Post A Comment: