Jumla ya Viongozi 406 wamepatiwa mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala Bora katika Halmashauri Nane za Mkoa wa Mwanza.
Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali na Mratibu wa Mafunzo hayo Adv Dorice Dario wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo katika wilaya ya Ukelewe Mkoani Mwanza ambapo amewataka viongozi hao kushusha elimu walioipata kwa wananchi wanaowaongoza.
“Wanavyotoka katika mafunzo haya basi wajitahidi kuitisha mikutano ya hadhara wawaelimishe wananchi hususani masuala ya Uzaelendo, Uraia pia na Wajibu na Haki zao katika jamii”
Wakili Dario Amesema wananchi wanapaswa kuelewa umuhimu wa kujitokeza kujiandilkisha na kupiga kura ili kwaajili ya kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika miaka mitano ijayo.
Naye Wakili wa Serikali, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Nuru Mwambuli, ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ,amesema imani yake mafunzo hayo yataleta tija na yatasaidia ulinzi na amani na kuimarisha utawala Bora katika mkoa wa Mwanza.
Mafunzo ya uraia na utawala yamehitimishwa katika mkoa wa Mwanza kwa makundi mbalimbali huku matarajio yakiwa ni kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwa makundi yaliopatiwa mafunzo hayo.
Ilielezwa kuwa mafunzo hayo yanatarajiwa kuzinduliwa katika Mkoa wa Tanga 14 Machi, 2025.
Post A Comment: