Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema Leo hii katika Makao Makuu ya Shirika hilo Ubungo Jijini Dar Es salaam Afisa Vipimo Mkuu kutoka Maabara ya Taifa ya Ugezi iliyopo TBS Bwn. Joseph Mahilla amesema ni muhimu sana kufanya Uhakiki wa Usahihi wa Vipimo ( Ugezi ) kwenye sekta ya Afya kwa maana ya Viwanda vinavyotengeneza madawa ( pharmaceutical Industries ).
Alisema wanatakiwa kufanya ugezi ili dawa zinazozalishwa ziwe na ubora unaotakiwa pamoja na maeneo yote yanayotoa Huduma za Afya kama Hospitali , Vituo vya Afya na Zahanati ili kulinda Afya za Watanzania kwa maana kifaa kinapofanyiwa Ugezi kitatoa majibu sahihi yatakayomwezesha Daktari au mtu yeyote katika Sekta ya Afya kutoa maelekezo sahihi kwa mteja.

" Mfano katika Hospitali , Vifaa vinapokua vimefanyiwa Ugezi vitatoa majibu sahihi ya Vipimo ambayo yatamwezesha Daktari kujua mgonjwa ana tatizo gani na kuchukua hatua stahiki za kupambana na ugonjwa husika kwa haraka sana, *daktari hutoa matibabu kutegemea Majibu yaliyotoka maabara, hivyo kama maabara imefanyiwa ugezi daktari atatoa matibabu sahihi kwa mgonjwa na kumhakikishia usalama wake, hii pia itapunguza upotevu wa muda na fedha kwa kufanya ufuatiliaji wa matibabu sehemu nyingine ama kupewa dawa wakati hakuna ugonjwa. Kufanya ugezi kunachangia maendeleo katika Jamii " amesema Mahilla .
Kwa upande wake Bi. Clara Mwinami Afisa Vipimo TBS ametoa wito kwa Hospitali ambazo hazijafanya Ugezi wa Vifaa katika Maabara zao kufika TBS kwa maana Uhakiki wa Usahihi wa Vipimo wa Vifaa vyao utawasaidia kuaminika kwa Huduma wanazozitoa .
Bi. Clara alimalizia kwa kusema kuwa Shirika la Viwango Tanzania TBS kupitia Maabara yake ya Metrolojia wanatoa Huduma ya Ugezi katika maeneo mbalimbali ambayo wana Umahiri na wamepata Ithibati katika Maabara zaidi ya Saba kutoka SADCAS kwa maana majibu wanayoyatoa ni sahihi na yanakubalika kote ulimwenguni.

Post A Comment: