Na Denis Chambi, Tanga.
MKUU wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani amelipongeza shirika la uwakala wa Meli Tanzania 'TASAC' kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali juu ya madhara yatokanayo na uchafuzi wa mazingira ya bahari ambayo yanaweza kuelekea athari za kiuchumi kwa mtu moja moja na Taifa kwa ujumla.
Balozi Dkt .Buriani ametoa wito huo wakati akifungua warsha ya mpango wa Taifa wa kujiandaa na mapambano ya umwagikaji wa mafuta katika bahati na mafuta ambapo amesema licha ya sekta ya uchumi kuathirika Kuna uwezekano mkubwa wa kupotea kwa viumbe vya bahari endapo juhudi mbalimbali hazitafanyika.
"Tunapaswa kutambua kuwa umwagikaji wa mafuta katika bahari na maziwa unaweza ukaathiri vyanzo vya mapato ya wananchi wetu wakiwemo wavuvi ,sekta ya utalii na usafirishaji itaathirika na hatimaye kuathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini Taifa kwa ujumla"
"Umuhimu wa hii semini ni mkubwa sana mafuta yatakapo mwagika watu tunategemea mazao ya baharini tutapata hasara Tanga tumeshaanza na kujikita katika zao la Mwani hivyo kukitokea dharura yeyote ni lazima kuwa tayari kukabiliana nayo hivyo ni lazima tujiandae kimafunzo, kivifaa.
Aidha Dkt Buriani ameipongeza TASAC kwa juhudi mbalimbali inazozifanya ikiwemo kutoa elimu jumuishi pamoja na ugawaji wa vifaa vinavyoweza kutumika wakati wa dharura akiwataka kuendelea kuongeza elimu hiyo kwa wadau wakiwemo wananchi sambamaba na kuwa na vifaa vya kutosha.
" Niwapongeze sana TASAC kwa vifaa ambavyo mmevitoa ili vifaa hivyo viweze kufanya kazi ni lazima tuwe na utaribu mzuri wa kuvitumia , ni lazima tuwe na vifaa vya kutosha na vifaa vyote view katika sehemu moja ili kuweza kufikiwa kwa urahisi ili oparesheni ikitokea iwe rahisi kuvipata tutakuwa na kikao cha wadau wote ili kuwaeleza ni wapi vifaa vinatumika na jinsi gani vitatumika"alisisitiza Dkt Buriani.
Alisema mkoa umejipanga kutoa elimu kwa wadau wote wa bahari pamoja na wananchi jinsi ya kutumia vifaa vitakavyotumika wakati wa kupambana na dharura ya umwagikaji wa mafuta hii ikilenga kuongeza zaidi ushirikiano katika kupambana na majanga pale yatakapotokea.
"Bandari ya Tanga hususani eneo la Chongoleani linatarajiwa kuwa lango kuu la kupokea na kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Chongoleani , ujenzi wa bomba hilo upo katika hatua za mwisho wenzetu tayari wameshaweka matank ya kuhifadhia mafuta, Mkoa una mashamba ya mafuta umeyatenga tumeshatenga vitalu ambapo wenzetu wa makampuni makubwa wana maeneo yao"
"Umuhimu wa hii semini ni mkubwa sana mafuta yatakapo mwagika watu tunategemea mazao ya baharini tutapata hasara Tanga tumeshaanza na kujikita katika zao la Mwani hivyo kukitokea dharura yeyote ni lazima kuwa tayari kukabiliana nayo hivyo ni lazima tujiandae kimafunzo, kivifaa.
Akizungumza Mkurugenzi wa idara ya usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira kutoka shirika la wakala Meli Tanzania 'TASAC' Leticia Mutaki amesema kuwa katika kuendelea kudhibiti na kupambana na athari za kimazingira katika bahati na mazingira shirika hilo linaendelea kutekeleza mpango wa kitaifa wa umwagikaji wa mafuta ambapo wamewahusisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi katika ngazi za wilaya hii ikiwa na lengo la kuongeza uelewa na itayati wa kupambana na majanga yanapotokea.
Aidha Mutaki amesema kuwa TASAC inaendelea kusiamamia usalama wa vyombo vyote vinavyofanya safari katika bahati kuhakikisha vinakuwa na ubora wakati wote hii ikiwa na lengo la kupambana na athari za kimazingira ambazo zinaweza kujitokeza na kuelekea athari kwa viumbe na rasilimali nyingine zinazopatikana baharini.
"Tunalojukumu la kusambaza na kujenga ufahamu kuhusu masuala ya mazingira ya bahari kuhusu usalama na ulinzi tunao mpango wa kitaifa wa kupambana na umwagikaji wa mafuta baharini huu ni mpango ambao unajumuisha taasisi za Serikali n hata mashirika binafsi na wadau wengine pamoja na wananchi ambao wanaweza kutusaidia pale kunapotokea tatizo hilo"
"Pia tunashughulika na usalama wa vyombo vinavyopita kwenye maji tunaviangalia ili visichafue mazingira yetu sasa hivi tuna suala la uchumi wa buluu ambao sasa hivi Duniani imeelekeza kwamba Kuna maliasili nyingi kwenye maji lazima tuvune kwa namna ambayo itaweza kuwa endelevu TASAC tunawajibu wa kuhakikisha kwamba maliasili zote zilizopo kwenye maji zinabaki salama"
"Tumekuja Tanga kujenga timu ili kama kunatokea bahati mbaya ya umwagikaji wa mafuta ili tuwe na watu ambao tunaweza kufanya nqo kazi katika kudhibiti athari zianazoweza kujitokeza kutokana na mafuta mabayo yanavuja ,tunao mradi wa EACOP ambao unaosafirisha mafuta kutoka kule Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania kama itatokea dharira yeyote ya umwagikaji wa mafuta ili kuweza kupunguza athari za kimazingira" alisema.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka shirika la bandari Zanzibar Abubakar Ally amelipongeze shirika la uwakala wa Meli Tanzania 'TASAC' kutokana na mafunzo hayo ambayo wameendelea kuyatoa kwa wadau wa usafirishaji wa majini pamoja na wananchi ambapo matokeo yake yameonekana na kufanikiwa kwa asilimia kubwa.
"Sisi kwa upande wa Zanzibar tunashukuru sana kushirikishaa katika masuala haya mpango wa Taifa wa kujiandaa na mapambano ya umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa niwapongeze sana TASAC kwa kuandaa mafunzo haya kwa sababu yanasaidia sana na tunaona mafanikio yake yanapotokea mambo kama haya" alisema.
Post A Comment: