Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekamilisha uchunguzi wa majalada 728 na kuwezesha kuchukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa sheria, ambapo kati ya majalada hayo 17 ni ya rushwa kubwa ambayo yanahusisha shilingi bilioni 11 na zaidi.
Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya TAKUKURU kwa mwaka 2023/2024 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Crispin Chalamila amezitaja chunguzi hizo kuwa ni katika mkataba wa upangishaji wa jengo la Ngorongoro Tourism Center kwa kodi ya shilingi bilioni 7.96 ambapo mpangishwaji wa jengo hilo alipangishwa chini ya bei iliyoelekezwa na bila kupata ridhaa ya bodi ya wakurugenzi.
Chunguzi hizo pia zimebaini kuwepo kwa vitendo vya rushwa na utakatishaji fedha wa shilingi bilioni 4.2 kwa watumishi wa kitengo cha Agency Banking cha Benki ya CRDB kutoka kwa Mawakala Wakuu (Super Agency) ili wasiwasitishie mikataba yao ya uwakala.
Vitendo vya rushwa na uchapishaji wa fedha kwa kushirikisha watumishi wa benki na watuhumiwa wengine ambapo bilioni 2.35 zilichepushwa na maafisa wa Benki ya ABC kupitia miamala iliyofanyika na kurejeshwa (Teller Reversal Entries), miamala ya kutuma pesa kutoka kwenye account kwa njia ya simu (mobile banking transfers), kuruhusu miamala iliyopitiliza iliyofanywa kwa kupitia huduma ya kadi ya malipo ya kabla (Card Over drawn in Connection with pre-paid card services).
Vitendo vya rushwa vilivyofanywa na kampuni ya NatGroup Limited kwa kushirikiana na watu wengine kama dhamana wakati wa kuchukua Credit Bond yenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 kutoka First Assuarence kwa lengo la kupata uwezo wa kununua petroli kwa njia ya mkopo kutoka kampuni ya usambazaji mafuta ya United Petrolium Limited.
Vitendo vya rushwa katika usambazaji wa vifaa vya umeme vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.01 katika bohari ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mwanza.
Post A Comment: