MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewafuturisha watoto wenye uhitaji wa kituo cha Chakuwama kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam na kuwapatia zawadi mbalimbali.

MWEZI mtukufu wa Ramadhan, unafundisha kufanya mambo mengi mema na kufuturisha wenye uhitaji, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru alisema, katika iftar hiyo iliyofanyika Alhamisi ambayo iliwahusisha pia Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF, Bi. Joyce Mapunjo, baadhi ya wajumbe wa bodi, Menejiment na watumishi wa Mfuko wa Mkoa wa Dar es Salaam.

""Tunamuomba Mwenyezi Mungu apokee ibada hii; Kwa niaba ya wanachama wa PSSSF ambao tunatunza amana zao na kuwekeza ili wanapostaafu waweze kulipwa vizuri tutaendelea kutoa sadaka na kushirikiana na jamii inayotuzunguka kama sehemu ya kutimiza wajibu wetu," alisema Badru..

Naye Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar ameipongeza kwa sadaka ya kufuturu pamoja na watoto wa Kituo cha CHAKUWAMA ikiwa ni pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali. 

"Kitendo hiki cha kukusanya watoto hawa na kutoa zawadi kwao, ni utekelezaji wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu ambaye amesisitiza upendo kwa watu wengine.














Share To:

Post A Comment: