Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amewataka Halmashauri ya Mtama kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa kulingana na thamani fedha iliyotolewa kwenye miradi husika
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amewataka Halmashauri ya Mtama kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa kulingana na thamani fedha iliyotolewa kwenye miradi husika
Na Fredy Mgunda,Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amewataka Halmashauri ya Mtama kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa kulingana na thamani fedha iliyotolewa kwenye miradi husika.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua uendelevu wa miradi hiyo, awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack , ametoa wito kwa menejimenti ya halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Mapema alipotembelea kukagua ujenzi wa shule na miundombinu hiyo ya elimu yenye thamani ya Bilioni 7.8 Kati ya fedha hizo, shilingi Bilioni 4.1 zinatoka serikali kuu, bilioni 3 kutoka kwenye Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), na milioni 719 kutoka kwenye Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
kutakuwa na ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mtakuja, ukarabati wa madarasa matano katika Shule ya Msingi Simana, ujenzi wa Shule ya Sekondari Navanga, na ujenzi wa Shule ya Amali Mpenda.
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya wavulana kanda ya Kiwalala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mahumbika, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Chiuta, na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mandwanga.
Post A Comment: