Na Denis Chambi, Tanga.
MKUU wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani amewaagiza wakuu wa wilaya , makatibu tawala na wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huo kutembelea na kujionea utendaji wa kituo cha sayansi cha stem Park ili elimu teknologia inayotolewa kwa wanafunzi wanqotembelea kituoni hapo iweze kutolewa ngazi zote.
Balozi Dkt Buriani amesema hayo wakati akifunga maadhimisho ya kusherehekea miaka mitano ya kuanzishwa kwa kituo cha sayansi cha Stem Park tangu kilipoanzishwa 2020 ambapo amepongeza elimu inayotolewa na wataalamu wa kituo hicho kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zilizopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Tanga ambayo imeonekana kuwa na tija kulingana na Maendeleo ya teknologia ya sasa.
"Tutaelekeza wakurugenzi, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wote wa wilaya ya mkoa wetu waje watembelee ili iende chini kwenye wilaya zetu zote na hatimaye ikawe ni mkombozi kwa vijana wetu wote, tunatamani hii fursa wanayoipata watu wa Tanga Jiji waipate na maeneo yote ya mkoa wetu"
Aidha amewataka wadau wa elimu mkoani humo Kwa kushirikiana na walimu na wazazi kuendelea kuwaunga mkono Sterm Park kwa kazi wanayoifanya chini ya shirika la Botner Foundation.
"Ni jambo kubwa mnalolifanya hapa na uwekezaji mkubwa mliouweka hapa matunda yake tumeuanza kuyaona , kupitia dira ya 2050 ambayo tunakwenda nayo kwa sasa , hiki kinachofanywa na kituo cha Sterm Park ndio mambo ambayo yako duniani kote maswala ya ubunifu , uhandisi na kupelekea ukuaji wa uchumi Dunia"
Aidha Dkt Buriani ameongeza kuwa Sera ya elimu inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imebeba maono ya kufanya Mapinduzi katika sekta ya elimu hapa nchini.
"Kutokana na maono ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba sasa tuanzishe shule za sayansi hasa kwa watoto wa kike, masomo ya sayansi hasa hisabati yalikuwa yanafelisha sana kipindi cha nyuma lakini kupitia mfumo huu wa kuwepo na shle za sayansi kumebadilisha sana mtazamo wa wanafunzi, masomo haya yamekuwa rafiki zaidi utaalam wa ufundiahaji umeongezeka".alisema.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho cha Sterm Park Luidiko Mhamelawa ameeleza kuwa miaka mitano tangu kuanzishwa kwa kituo hicho imeleta mabadiliko chanya husausan kwa wanafunzi wa shule za msingi ambao wamekuwa wakiongezeka na kuhamasika kujitika tatika masomo ya sayansi.
Amesema mwenendo huo kituo kina kazi ya ziada ya kufanya kwa miaka mingine ijayo kuhakikisha mabadiliko ya sera mpya ya elimu iliyojikita kwenye masuala ya teknologia inawapa nguvu na matumaini kuwa ushirikiano wao pamoja na wadau utazidi kuwa na mafanikio.
"Tunaposherejekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa kituo cha Sayansi cha Sterm Park hapa Tanga imekuwa ni miaka ya furaha sana tumefikia watoto wengi zaidi"
"Kwa miaka mitano inayokuja tunapata hamasa kubwa kupitia sera mpya ya elimu ambayo ina msisitizo kwenye kujivunza kwa vitendo na matumizi ya teknologia katika ufundishaji sasa sera hii inatupa nguvu sisi kuona kuwa tunaweza kuwa washirika wakubwa wa Serikali kwaajili ya utekelezaji wa sera hii mpya" alisema Mhavilawa.
Alisema ili kupanua wigo wa elimu wanayoitoa kituoni hapo wameanziaha Klabu mbalimbali katika shule za msingi na sekondari ambapo mpaka sasa 22 wakitarajia kufikia mkoa mzima wa Tanga.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa uwepo wa kituo hicho jijini Tanga na matokeo yake ambayo yameanza kuonekana kimewavutia wadau wengine kutoka katika wilaya na mikoa mingine alisema kuwa ushirikiano mzuri utakaowekwa baina yao na Serikali utasaidia kuanzishwa vituo vingine hapa nchini.
"Kwa sasa tumeshavuka malengo yetu ya awali tunategemea tufikie Tanga nzima lakini hiki kituo kumekuwa na mvuto kwa mikoa mingine kupitia wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali wote wanatamani kuwa na kituo kama hiki kwahiyo tunategemea ushirikiano mzuri wa Serikali ili kueneza elimu hii ya kujifunza kwa vitendo " alisema Mkurugenzi huyo.
Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya Jiji la Tanga Naibu Meya wa Baraza la madiwani Rehema Mhina amepongeza uwepo wa kituo hicho ambao umeanza kuzaa matunda huku akiwaahidi kuendelea ushirikiano baina yao na kituo.
"Niwapongeze sana watekel zaji wa mradi huu ambao umeanza kuleta matokeo ya kuonekana tumejitahidi sana kuhamasisha watoto kupenda masomo ya sayansi katika Jiji letu la Tanga"
Amewataka wazazi na walezi kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa kuwahimiza watoto wao kupenda masomo ya sayansi sambamba na kupambana na vitendo vya ukatili.
Post A Comment: