MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mh.  Anamringi Macha ameweka jiwe la msingi Shule mpya ya sekondari Bumva, Kijiji cha Bumva Kata ya Segese Halmshauri ya Wilaya ya Msalala iliyojengwa kwa gharama ya Sh. Milioni 603,890,563/=ambayo inatarajia kupokea wanafunzi zaidi ya 100 kutoka shule za sekondari ya Mwalimu Nyerere na Segese wanaotoka katika  vijiji vya Bumva, Busongo C, Wisolele na  Senta mashariki kwa vitongoji vya Misungwi na Itembe.


Mkuu wa mkoa Mh. Anamringi Macha amesema, Serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha na kusogeza miundombinu ya elimu kwa wananchi kusudi kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanapata elimu na sio kuwatumikisha mashambani na kuchunga mifugo. Amesisitiza Miundombinu hiyo iendelee kutunzwa na kuzingatia suala la utunzwaji wa Mazingira ikiwemo upandaji wa miti.


Katibu Tawala wa Mkoa CP. Mhe.  Salum Hamduni amesema Serikali inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali. Zaidi ya Bilioni 6 ndani ya Mkoa wa Shinyanga zimetolewa ambayo inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Bumva inayoendelea kujengwa kwa kiasi cha Sh. Milioni 603,890,563/=  na hivyo kuweza kusogeza huduma ya upatikanaji wa elimu karibu na wananchi.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bi. Rose Manumba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha  za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo ikiwemo shule ya Sekondari Bumva ambayo inakwenda kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu na utoro sugu.


Aidha DED Manumba amewataka Watumushi wa Halmashauri hiyo kuendeleza jitihada na kasi ya usimamizi na utekelezaji wa miradi mingine inayoendelea kutekelezwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora wa mradi na thamani ya pesa ionekane.


Akitoa taarifa ya ujenzi wa sekondari hiyo leo tarehe 03 Machi 2025 Mkuu wa Shule ya  sekondari ya Mwalimu Nyerere, Bw. Kafuru Songoro amesema, kukamilika kwa shule hiyo ya Bumva  kutasaidia wanafunzi kuondokana kuondokana na msongamano madarasani na kusaidia kupunguza mimba za utotoni. Shule mpya ya Sekondari Bumva ina majengo yafuatayo: Jengo la utawala, vyumba nane vya madarasa, Ofisi ya walimu, jengo la Tehama na Maktaba, Maabara(3), vyoo na kichomea taka.


Mh. Anamringi Macha ameshiriki zoezi la upandaji miti na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika suala zima la utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yao.


Imewasilishwa na : 

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Msalala DC


























Share To:

Post A Comment: