Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Machi 09, 2025 amezindua mradi mkubwa wa maji Same-Mwanga-Korogwe unaogharimu takribani Shilingi Bilioni 3 zilizowezeshwa na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Mradi huo ambao utanufaisha wananchi zaidi ya 300,000 katika Wilaya za Same na Mwanga, mkoani Kilimanjaro utasaidia kupunguza changamoto ya maji kwa wananchi wanaoishi ukanda wa tambarare katika wilaya hizo.
Ujenzi wa mradi huo kwa awamu ya kwanza umekamilika tangu Julai 2024 na hadi kufikia Machi 2025, wakazi wapatao 300,000 wa wilaya za Same na Mwanga wanapata huduma nzuri ya maji safi, salama na ya kutosheleza mahitaji.
Kwasasa Mamlaka ya Maji inaendeleza mtandao wa mabomba na kufanya maunganisho ya maji kwa wakazi na kujenga vituo vya kuchotea maji, kukarabati na kuboresha miundombinu ya zamani ambapo kufikia April mwaka huu, huduma ya maji inatarajiwa kuwafikia wananchi wengi zaidi wa Mjini Same na Mwanga na hivyo kufikia lengo la serikali la asilimia 95 maeneo ya Mijini.
Wakati wa Uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi huo na kusimamia utekelezaji wake, akiahidi shukrani ya wananchi wa Mkoa huo kuwa ataipata wakati wa uchaguzi mkuu kwa kumchagua kwa kishindo aweze kutetea nafasi yake.
Post A Comment: