Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini kwa jitihada zake za kuongeza idadi ya shule zinazotoa masomo ya amali, ambapo hatua hiyo ni ishara njema ya kanisa kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo, hususan kwenye sekta ya elimu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam tarehe 21 Machi 2025 katika hafla hiyo, Prof. Mkenda alisisitiza kuwa Ujenzi wa Majengo hayo yatatoa fursa zaidi za elimu kwa wanafunzi na kuhakikisha idadi kubwa ya watoto wanapata nafasi ya kusoma.
Aidha, alitoa wito kwa shule zote za serikali na zisizo za serikali kuwahamasisha waliowahi kusoma katika shule hizo kurudi na kutoa mchango wao kwa ajili ya maendeleo ya shule walizosoma, akisisitiza mshikamano katika kuwekeza kwenye elimu bora kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Post A Comment: